BUENOS
AIRES, ARGENTINA
LIONEL MESSI
ametangaza kurejea katika timu ya taifa ya Argentina inayojiandaa kuwania
kufuzu kwa Kombe la Dunia septeamba, akimaliza muda mchache aliotangaza kustaafuy
soka la kimataifa.
Messi, 29,alitangaza
kustaafu baada ya kukosa penalti katika mchezo wa fainali wa Copa America- na
kuifanya Argentina kupoteza taji kubwa la tatu mfululizo.
"Nimeona kuna
matatizo mengi katika soka la Argentina na sikutaka kutengeneza mengine," alisema
Messi, ambaye ametajwa katika kikosi cha wachezaji 18 kitakachopambana na Uruguay na
Venezuela.
Katika waraka wake wa
Ijumaa alisema :" Sitaki kusababisha madhara, katika nchi yangu, lengo
langu ni kuweza kusaidia kwa njia yoyote ninayoweza."
Messi ambaye ni
mfungaji wa muda wote wa Argentina anaongoza kwa kufunga mabao 55 katika
michezo 113, alilishutumu shirikisho la soka la Argentina (AFA) siku chache
kabla ya fainali ya Copa Amerika.
Straika huyo wa Barcelona
alifanya hivyo baada wachezaji wa Argentina kuteseka kwa kucheleweshwa ndege na
matatizo ya muda mrefu ya kutafuta wapinzani kwa ajili ya mechi za maandalizi.
"Kuna mambo
mengi katika soka la Argentina ambayo yanatakiwa kuwekwa sawa. Lakini ninaona
ni bora kusaidia nikiwa ndani kuliko kusimama nje na kuponda," ulisema
walaka huo.
"Mambo mengi
yalipitakatika kichwa change siku ya
fainali (Copa Amerika). Na nilichukulia makini
uamuzi wa ngu wa kuondoka katika timu. Lakini ninaipenda jezi na nchi yangu sana.
"Nataka
kuwashukuru mashabiki wangu wote waliotaka niendeleae kuitumikia Argentina.
Ninamatumaini tunaweza kuwapa furaha muda si mrefu."
Wakati ikiwa siku ya
mwisho ya kutaja kikosi kitakachoshiriki hatua ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, kocha
mpya wa Argentina, Edgardo Bauza amekuwa na uhakika kwmaba Messi atabadilisha
uamuzi wake na kurudi katika timu, na hiyo imeaminika baada ya Messi
kuwasilisha barua.
Kocha Bauza amechukua
kibarua cha kuinoa Argentina baada ya kocha wa awali Gerardo Martino kujiuzulu
mwezi uliopita.
Kocha huyo alienda
Hispania kukutana na wachezaji wa Argentina wanaoitumikia Barcelona Alhamisi na
kuwahakikishia kutakuwa na utaratibu pamoja na machafuko yanayoendelea katika
shirikisho la soka.
Alisema
hakumshinikiza Messi kuangalia upya uamuzi wake wa kustaafu soka na
walizungumza soka tuna straika huyo, lakini alidai Messi alitaka kurudi.
"Hakuna shaka
katika akili yangu kwamba alitaka kurudi kuitumikia timu ya taifa," Bauza
aliwaambia waandishi wa habari Argentina "Nilimuona akiwa na hamu kubwa ya
kurejea."
Argentina inajiandaa kufuzu
Kombe la Dunia hapo Septemba dhidi ya Uruguay na Venezuela baada ya kutolewa
katika makundi ya Olimpiki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1964.
AFA limekuwa
likiongozwa na Julio Grondona tangu miaka ya 1970s, limeingia katika mtikisiko
baada ya kifo chake 2014.
Mwezi Juni, Shirikisho
la Soka la duniani (Fifa) lilitaja Kamati kuendeleza mambo yake, na kutakiwa
kufanya uchaguzi Julai 2017.
Mkongwe wa Argentina,
Diego Maradona aliai machafuko ndani ya shirikisho yalikuwa ni taasisi na Messi
alikuwa sawa kutoa maoni yake.
Hapa
ni kikosi cha Argentina:
Makipa: Sergio Romero (Manchester United),
Mariano Andujar (Estudiantes) na Nahuel Guzman (Tigres).
Mabeki: Facundo Roncaglia (Celta), Mateo
Musacchio (Villarreal), Ramiro Funes Mori (Everton), Emmanuel Mas (San
Lorenzo), Marcos Rojo (Manchester United), Martin Demichelis (Espanyol), Pablo
Zabaleta (Manchester City), Gabriel Mercado (Sevilla) na Nicolas Otamendi
(Manchester City).
Viungo: Matias Kranevitter (Atletico Madrid),
Javier Mascherano (Barcelona), Lucas Biglia (Lazio), Augusto Fernandez
(Atletico Madrid), Ever Banega (Inter), Javier Pastore (PSG), Erik Lamela
(Tottenham), Nicolas Gaitan (Atletico Madrid) na Angel Di Maria (PSG).
Mastraika: Lionel Messi (Barcelona), Angel Correa
(Atletico Madrid), Lucas Pratto (Atletico Mineiro), Sergio Aguero (Manchester
City), Paulo Dybala (Juventus) na Lucas Alario (River).
Post a Comment