0


MANCHESTER, ENGLAND
PAULO POGBA amepewa ruhusa na timu yake ya Juventu kufanya vipimo vya afya klabuni Manchester United na klabu zote mbili zimethibitisha hilo.
Ripoti zinasema Pogba, 23, alikuwa katika hatua ya kukamilisha zoezi la kufanya vipimo vya afya, United Jumapili kabla ya kukamilisha uhamisho wake.
Msemaji wa Juve  alifafanua kwamba kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amepewa ruhusa kufanya vipimo vya afya lakini  msemaji huyo alishindwa kuweka wazi kwamba tukio hilo litafanyika lini kwa sababu lipo chini ya United.
United ilitoa taarifa iliyosomeka: "Paul Pogba amepewa ruhusa ya kufanya vipimo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus na kujiunga na Manchester United."

Pogba akiwa na Drake
Jumamosi, kocha wa Juventus, Massimilano Allegri alisema Pogba aliyeachwa na United miaka minne iliyopita, ataripoti Turin  Jumapili kwa ajili ya kujiunga na wachezaji wenzake kufanya mazoezi.
Baada ya ushindi wa mchezo wa kirafiki dhidi ya West Ham Jumapili Mchana ambapo Juve ilishinda 3-2, Allegri alisema: "Nilisema jana kuhusu Pogba. Ndio kwanza tumemaliza mechi. Sijui zaidi.
"Kesho tutakuwa na uhakika kama Pogba bado ni mchezaji wa Juventus au la."
Mwezi uliopita chanzo cha uhakika kilisema United na Juventus zilifikia makubaliano juu ya dau la Pogba ambalo limeweka rekodi ya dunia.

United tayari ilikubali kuilipa Juventus Pauni 101.3 ( Uero120) lakini kulikuwa na majadiliano kuhusa ada zaidi.
Baada ya majadiliano hayo, imefahamika kwamba United italipa Pauni 95 milioni (Euro112.6m) kama ada ya uhamisho kwa ajili ya mchezaji huyo  pamoja na Pauni 20 milioni (Euro 23.7m) ada ya wakala.
Kiasi hicho ambacho klabu zilitakiwa kumlipa wakala wa Pogba, Mino Raiola, kilikuwa kikwazo kikubwa cha mazungumza hayo, ambapo Juve ilisisitiza ilitakiwa kulipwa yote na klabu hiyo ya Old Trafford.
Lakini pande hizo tatu zikapingana, na United ilikuwa ikitaka kupunguziwa kiasi cha kumlipa Raiola na Juve ilikuwa ikijipanga kulipa kodi ya dili hilo.

Post a Comment

 
Top