0


LONDON, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC NOMAAA. Zikiwa zimebakia siku sita kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu tayari mambo mawili yako wazi.
Leicester City itaendelea kutupa kile kilichotupa msimu uliopita. Nguvu, mashambulizi ya kushtukiza na mabao ya kushtua.

Manchester United, kwa upande mwingine, tayari imeonakana kuwa na mabadiliko.
Man ilikuwa tofauti na ile iliyokuwa chini ya kocha Louis van Gaal katika mchana wa kuwania taji la Ngao ya Jamii katika Uwanja wa Wembley.

Zikiwa zimebakia dakika saba kumalizaka kwa mchezo huo Zlatan Ibrahimovic, aliunganisha kwa ujanja krosi kwa kufunga kwa  kichwa  na kumwacha kipa wa Leicester Kasper Schmeichel akiwa hana la kufanya.
Na kuwa bao la kwanza la ushindi katika mchezo wa mashindano ambalo kabla ya kuzama wavuni mpira uligonga mlingoto wa goli.

Ndio, Ibrahimovic alikuwa amezidi. Lakini sehemu mbaya aliyokuwa amekaa beki na nahodha wa Leicester, Wes Morgan wakati Antonio Valencia akipiga krosi kutoka upande wa kulia ulimweka Ibra sehemu salama.

Lingard akishangilia bao la kwanza.
Huo ulikuwa ushindi mwembamba na Leicester walipigana kiume. Vijana hao wa kocha Claudio Ranieri walipambana kusawazisha bao lililofungwa na Jesse Lingard.

Jamie Vardy aliyatumia vizuri makosa ya kiungo, Marouane Fellaini ambaye alirudisha pasi mbovu ya nyuma na kusawazisha bao hilo.

Post a Comment

 
Top