MANCHESTER,
ENGLAND
ZLATAN
IBTRAHIMOVIC (pichani juu) amechaguliwa kuwa makamu nahodha na bosi wa Manchester United,
Jose Mourinho.
Straika huyo mwenye umri wa miaka
34- atapewa kitambaa cha unahodha kama Wayne Rooney na Michael Carrick hawatakuwapo
uwanjani.Ibrahimovic aliwahi kuwa nahodha alipokuwa akiitumikia timu ya taifa ya Sweden (kwa sasa amestaafu) katika sehemu kubwa ya michezo ya kimataifa na ana uzoefu wa kuongoza timu.
Habari kutoka ndani ya United zinasema: “Baadhi ya wachezaji, hasa vijana, wanamhofia Zlatan.
“Anakuwa na mvuto kila anapokuwapo na watu wanamwangalia baada ya kufanikiwa kupitia kazi yake.
“Ana uzoefu kwa kiasi kikubwa na bila shaka anaonekana kuwa kama nahodha pindi wachezaji wengine wanapokosena uwanjani.”
Ibrahimovic alisafirisha magari yake yenye thamani ya Pauni 1.5 milioni baada ya kuondoka katika hoteli aliyokuwa akiishi Ufaransa.
Alitafuta nyumba ya kupanga maeneo ya Manchester Radisson kwa ajili yake na familia yake baada ya wiki alipotua Manchester.
United inamlipa bili ya Pauni 20,000- kwa mwezi ikiwa ni kosdi ya nyumbwa mbali na mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.
Pia ana gari jekundu aina ya Ferrari Enzo na Porsche Spyder yakiwa ni baadhi ya magari yake mengine aliyoyanunua Paris.
Ibrahimovic alijiunga na United akitokea PSG uhamisho wa bure katika usajili wa majira haya ya joto.
Alifunga mabao 113 katika mcihezo 122 akiwa na miamba ya Ufaransa ndani ya misimu minne.
Post a Comment