0


LEICESTER, ENGLAND
RIYAD MAHREZ amekuwa nyota wa pili wa Leicester City kuwa na nia ya kusajili Arsenal kisha kubadali mawazo na kumwaga wino kuwatumikia Mabingwa wa Ligi Kuu England.
Mahrez mwenye umri wa miaka 25  amehusishwa kwa kiasi kikubwa na uvumi wa kuhamia The Gunners. Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa mchezaji mwenzake, Jamie Vardy, Mahrez ameamua kubaki uwanjani King Power  na kusaini mkataba wa miaka minne utakaomfanya kuwa na klabu hiyo hadi Juni 2020 wenye thamani ya Pauni100,000-kwa wiki.

Habari hiyo itakuwa faraja kubwa kwa kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri, ambaye alimpoteza kiungo wake N’Golo Kante alkiyejiunga na Chelsea kwa dau la Pauni 32 milioni mapena katika dirisha la usajili wa majira ya joto. 
Mwenyekiti wa Leicester City ‘Mbweha’, Vichai Srivaddhanaprabha alifanya mazungumzo ya kina na Mahrez na kumweleza nia yake ya kutaka kukibakisha sehemu kubwa ya kikosi kilichoishangaza dunia kwa msimu uliopita. 
Muargeria Mahrez, Mchezaji Bora wa kulipwa PFA wa mwaka, aliifungia timu yake mabao 17 na alitengeneza asisti 11 katika msimu huo wa kushangaza chini ya kocha Ranieri.
Alisajiliwa kutoka katika timu ya Ufaransa ya Le Havre mwaka 2014 wakati klabu hiyo ikicheza Championship. 
Inafahamika  kwamba mkataba ambaoa ameiingia hauna kifungu kidogo kinachoweza kumruhusu kuondoka kwa ada inayowekwa wazi.

Katika walaka uliotolewa katika mtandao wa Mbeha hao Jumatano usiku, ulisema Leicester inafuraha kutangaza Mahrez kuongeza  mkataba mpya.
Sasa Mahrez na Vardy wanajiandaa kucheza na Arsenal Jumamosi. 
Leicester iko mbioni kumwandalia dili jipya beki wake wa kushoto ambaye ni nyota wa kimataifa wa Ghana, Jeffrey Schlupp ili kumzuia kujiunga na West Bromwich Albion ambayo inalenga kumnasa.

Post a Comment

 
Top