0


VALENCIA, HISPANIA
SHKODRAN MUSTAFI anafanya mazoezi pake yake wakati akiisubiri Arsenal kumaliza taratibu za uhamisho.
Beki huyo wa Kijerumani a
mevutiwa na mpango wa kujiunga na Gunners na kwa mujibu wa wawakilishili wake,  ameshakubaliana masuala binafsi na klabu hiyo ya London Kaskazini ili aweze kutua Emirates.
Wakati Valencia ikisisitiza haipo kwenye majadiriano na klabu yoyote kuhusu beki huyo mwenye umri wa miaka 24.
Chanzo kutoka katika klabu hiyo ya Hispania kimeweka wazi kwamba huenda kuna matatizo lakini Arsenal inapaswa kufikia Euro 25 milioni (Pauni 21milioni) inayotakiwa.

Beki huyo wa kati aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani anafanya mazoezi peke yake ili kurudi katika ubora wake.
Lakini Valencia, iliyokuwa imejipanga kutinga Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya msimu huu lakini imeshindwa kupata nafasi hiyo, inawauza baadhi ya nyota wake hata baada ya kumpiga bei Andre Gomes kwa Pauni 45 milioni kwa Barcelona na haitaki beki wake huyo wa kati apate majeraha.

Kama haitoshi Barca bado inawahitaji fowadi, Paco Alcacer na kipa Diego Alves kutoka katika klabu hiyo. Valencia imekosa  kuungwa mkono na mashabiki wake.
Beki Mustafi amekuwa akivutiwa na Ligi ya Bundesliga kitu ambacho kitaifanya Arsenal kuongeza spidi ya kumnasa.

Post a Comment

 
Top