MANCHESTER, ENGLAND
PAUL POGBA atacheza dakika chache
katika mchezo wa Manchester United dhidi ya Southampton uwanjani Old Trafford
Ijumaa usiku, Kocha Jose Mourinho amethibitisha hilo.Kiungo Pogba, 23, anajipanga kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England tangu aliporudi kujiunga na United katika usajili huu wa majira ya joto uliovunja rekodi ya usajili kwa Pauni 89.3 milioni akitokea Juvuntus kwa dili la miaka minne.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifungiwa kuitumikia timu yake hiyo katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth, Jumapili iliyopita.
"Tulicheza dhidi ya Leicester (katika mchezo wa Ngao ya Jamii) tukiwa na wachezaji waliofan ya mazoezi kiasi zaidi yake na tukashinda mchezo ule (2-1) tukiwa katika kuwaboresha na kuharakakisha mchakato," Mourinho aliimbia Runinga ya Manchester.
"Na kwa Paul, anaonekana kuwa sawa – hakuwapo hata kwa dakika moja kwenye mechi za maandalizi, lakini karibu wiki mbili amefanya kazi nasi, kuna wakati katika makundi, wakati mwingine peke yake, na yuko vizuri kucheza kwa dakika kadhaa."
Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, kocha huyo wa United aliongeza kwamba Pogba anahitaji muda kuelewa upande wake anaopaswa kucheza, lakini mfumo wa uchezaji wa timu hautabadilika kwa kiasi kukubwa.
"Ameushika kwa urahisi na haraka kwa sababu anaijua klabu, anamjua kila mmoja," alisema Mourinho.
"Haitaji muda mrefu wa kukabiliana, lakini anahitaji muda wa kujenga hali yake na kufahamu jinsi ya timu inavyocheza na vile atakavyofiti na hali hiyo.
Jose Mourinho
"Hatutacheza watano nyuma kwa
kuwa Juventus inacheza watano. Hatutakwenda kwenye mabadiliko makubwa. Lakini, ndio, kuna mabadiliko katika maelezo na kwenye
michezo ambayo tutatakiwa kubadilika."Mourinho pia alithibitisha kwamba beki wa kati Chris Smalling anaweza kuwepo katika mchezo huo dhidi ya Southampton.
Beki huyo wa kimataifa wa England aliumia katika michezo ya mwanzo wa msimu kisha akasimamishwa katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Bournemouth.
Post a Comment