LEICESTER,
ENGLAND
LEICESTER
CITY imegoma kumuuza winga wake, Riyad Mahrez mwezi huu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria yuko tayari kujifunga
kwa mkataba mpya, chanzo cha ndani ya klabu kimeweka wazi.
Mustakabali
wa Mahrez ndani ya Leicester ulikuwa shakani katika dirisha hili la usajili wa
majira ya joto kwa kuhusishwa na Arsenal na Chelsea.
Chanzo
hicho kimesema kuwa Mahrez alikuwa tayari kuondoka Leicester katika usajili huu
wa majira ya joto, lakini klabu imekataa kumruhusu kuondoka kama ilivyokuwa kwa
N'Golo Kante aliyejiunga na Chelsea.Bosi wa Foxes, Claudio Ranieri amesema
Jumatano kwamba: "Kante alikuwa na kifungu kinachomruhusu kuondoka ambacho
Chelsea wamekilipia, lakini Riyad hana kifungu kama hicho hivyo ataendelea kuwa
nasi.
"Mahrez
alipewa ofa ya mkataba mrefu lakini ameukataa, pamoja na kwamba ofa ya mkataba
wa miaka minne bado iko juu ya meza.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alijiunga na Leicester akitokea Le Havre
mwaka 2014, amekataa kusaini mkataba huo
mpya mpaka kifungu kinachoweza kumruhusu kuondoka kiingizwe hapo ndipo anaweza kumwaga wino.Mahrez
atakuwapo kwenye kikosi kitakachoanza cha Leicester ambacho kitacheza mchezo wa
ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City wikiendi
hii.
Post a Comment