LONDON,
ENGLAND
SHKODRAN
MUSTAFI yuko tayari kutua Arsenal. Wakala wa beki huyo wa Valencia, Ali Bulut amesema
mteja wake ameshakubaliana na Arsenal lakini bado klabu hizo zinajadiliana
kuhusu ada ya uhamisho.
Bulut
alisema kwamba beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24, amekubaliana
maslahi binafsi na yuko tayari kutua uwanjani Emirates.
"Shkodran
na Arsenal wameshakubaliana. Kilichobaki ni klabu tu kufukia mwafaka wa ada ya
uhamisho," alisema Bulut.
Habari
zinasema kwamba Arsenal ilikuwa tayari kutoa dau linalokadiriwa kufikia Pauni 20 millioni kwa
ajili ya Mustafi, na wengine wakidai kwamba inaweza kufika Pauni 30 milioni.
Arsenal
inahitaji kupata beki wa kati baada ya mabeki wake Per Mertesacker na Gabriel
Paulista kuumia kipindi cha maandalizi ya msimu na watachukua muda mrefu kupona.
Hata
hivyo, Kocha Arsene Wenger alisema hatarajii
kumleta beki mpya kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool,
Jumapili.
Kocha Wenger
Mustafi, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia
mwaka 2014 na aliitumikia nchi yake katika michuano ya Euro 2016, uwezoefu wake
utamfanya Wenger amfanye kuwa patna wa Laruent Koscielny, ambaye anatarajiwa
kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Liverpool.
Beki
huyo ameshatakiwa na Arsenal na hata Manchester United kwa nyakati tofauti.
Post a Comment