HE! POGBA AFUNGIWA MANACHESTER UNITED
PAULO POGBA ambaye ametua Manchester United na kuanza mazoezi hatacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Bournemouth, Chama cha Soka (FA) kimethibitisha.
FA imesema Pogba aliyesajiliwa kwa dau lililovunja rekodi ya dunia amefungiwa kuitumikia timu yake mchezo wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, amerudi Old Trafford akitokea Juventus katika usajili uliofanyika msimu huu wa majira ya joto kwa Pauni 89.3 milioni, ikiwa ni miaka minne baada ya Old Trafford na kwenda Turin kwa fidia ya Pauni 800,000.
Hata hivyo, kiungo huyo anapaswa kusubiri hadi mchezo wa pili wa United kwani hataweza kuitumikia timu yake katika mchezo dhidi ya Bournemouth utakaopigwa Jumapili.
Mfaransa huyo amefungiwa baada ya kupata kadi mbili katika mchezo wa Coppa Italia msimu uliopita, kadi ya pili aliipata katika mchezo wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AC Milan katika fainali.
FA imethibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba kusimamishwa kwake kumehamishiwa katika Ligi ya Kuu England na kumfanya kutoshiriki katika mchezo wake wa kwanza chini ya Kocha Jose Mourinho.
Habari kutoka ndani ya United zinasema kulikuwa na uwezekano mdogo kwa Pogba kuanza katika mchezo huo dhidi ya Bournemouth.
Kocha Mourinho alipanga kumtompanga, Pogba ambaye alicheza mchezo wake wa mwisho katika kikosi cha Ufaransa kilichopoteza fainali ya Euro 2016 kwa Ureno Julai 10, akicheza dakika 120 za mchezo huo jijini Paris na wenyeji kufungwa 1-0.
Post a Comment