0
MACHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO ameweka wazi kwamba Ligi ya Mabingwa Ulaya ni bure bila ya uwepo wa Manchester United msimu huu.
Pamoja na kushinda taji hilo mara mbili kwa miaka ya hivi karibuni, na kuvuna kwa mara ya tatu kwa jumla, United imeshindwa kufuzu mashindano hayo ya klabu za Ulaya mara mbili ndani ya miaka mitatu.
Kocha mpya Mourinho anataka kuiondoa tabia hiyo msimu huu wa Ligi Kuu na Mreno huyo anadai wasiwasi kwamba Ligi ya Mabingwa itapoteza mvuto wake bila ya uwepo wa klabu hiyo ya Old Trafford.

“Man United inapaswa kuwa bingwa wa Ligi ya Mabingwa,” alisema. “Nadhani Ligi ya Mabingwa haina kitu pindi inapokosekana Man United.
“Hebu fikiria Ligi ya Mabingwa bila ya Man United, Real Madrid na  Barcelona. Kuna baadhi ya klabu zinaifanya isiwe Ligi ya Mabingwa kwa kukosekana kwao. Hiyo ni Man United na utamaduni wake halisi.”
Kushika nafasi ya tano mwishoni mwa msimu uliyopita ni matokeo ya Mashetani Wekundu kushiriki Europa League msimu huu – Matokeo ambayo Mourinho anataka kuyafanyia mabadiliko siku za usoni kwa kushinda mataji.
“Sitakuwa na furaha kwa kumaliza katika nne bora,” aliongeza.

“Nita furahia hilo lakini natarajia kufanya mageuzi makubwa katika soka letu – kwa kufungua milango kwa miaka kadhaa ijayo kurudisha mataji.
“Sitaki kwenda kwa wachezaji na kuwaambia ‘tumalize kwenye nne bora’ – tujaribu kushinda kila mchezo, hususan katika nchi hii – katika muda huu ambao ni mgumu kwa kila mmoja.

“Lakini tukiwa na kianzia hicho, acha twende tukashinde kila mchezo. Lakini klabu kama yetu, tunatakiwa tuwe na desturi hiyo.” 

Post a Comment

 
Top