RIO DE
JENAIRO, BRAZIL
NEYMAR
anaweza kuacha kuitumikia timu ya taifa ya Brazil kama alivyofanya Lionel Messi
kwa Argentina, bosi wa soka wa Brazil ameonya.
Bosi Rogerio Micale amewataka
mashabiki ambao ni wenyeji wa michuano hiyo ya Olimpic kuwa nyuma ya nyota huyo
katika mchezo dhidi ya Denmark ambao Blazil lazima ishinde.Mchezo huo utakaotoa hatma ya Brazili katika mashindano hayo utafanyika usiku wa Jumatano (kwa Afrika Mashariki).
Kama ilivyokuwa kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014, vijana hao wacheza staili ya Samba wako katika hatari ya kujiokoa kwenye hatari ya kung’olewa na wanahitaji ushindi ili kuweza kupata medali yoyote ile.
Neymar na wachezaji wenzake wamekuwa wakizomewa na staa huyo amekuwa akishutumiwa kutokana na kuonesha kiwango kidogo na uongozi wake mbaya.
Lakini Micale alisema Neymar anastahili heshima na anaweza kujiuliza kuhusu matarajio yake ya kuitumikia nchi kama hataipata.
Kocha huyo wa Brazil alisema: “Kama hatutawaheshimu wachezaji wetu, hawatataka kuwa pamoja nasi skiku za baadaye.
“Neymar atakuja kuwa mchezaji bora wa dunia, tunahitaji kumheshimu.
"Bado ni kijana. Nafahamu kwamba kuna wakati anakuwa na tabia ambazo hazitupendezi, lakini katika umri wake, hatupaswi kufanya vitu anavyovifanya na kuwa na kila kitu ambacho anacho?"
Timu ya taifa ya Brazil ililazimishwa sare ya bila ya kufungana dhidi ya Iraq na Afrika Kusini na inaweza kutolewa kwenye hatua ya makundi kama haitashinda dhidi ya Denmark.
Miaka miwili iliyopita Brazil ilifungwa na Ujerumani mabao 7-1 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Nyota wa Argentina, Lionel Messi alichukua hatua ya kutoitumikia timu yake ya taifa baada ya kipigo cha kwenye fainali ya Copa Amerika dhidi ya Chile.
Sasa kuna wasiwasi kwamba Neymar anaweza kufuata njia hiyo ya mchezaji mwenzake huyo wa Barcelona .
Hiyo inaweza kutokea baada ya shabiki mmoja kijana alipoliondoa jina la nyota huyo wa Barcelona katika jezi na badala yake kuliweka jina la Marta.
Marta ni mchezaji wa mkongwe wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazili ambaye yuko kwenye kiwango kizuri
"Neymar ni kijana mwenye umri wa miaka 24-year ambaye bado hajakomaa.
"Kwa ujumla mchezaji huyo atakuwa vizuri zaidi kimwili na kiakili akiwa na umri wa miaka 28. Neymar amekuwa akipewa presha ya uongozi tangu alipokuwa na umri wa miaka 17."
Na kiungo Renato Augusto aliongeza kwamba kuzomewa kunamwathiri Neymar.
Alisema: " Bado ana ujasiri, lakini hana furaha na kile kinachoendelea."
Post a Comment