LIVERPOOL, ENGLAND
JURGEN KLOPP amesema hana uhakika
kama straika wake Daniel Sturridge ataweza kucheza mchezo wa ufunguzi wa Ligi
Kuu England dhidi ya Arsenal.Sturridge alikosa michezo miwili ya kirafiki ya maandalizi ya msimu ya Liverpool kutokana na tatizo la nyonga.
Klabu imesema amekosa mchezo wa uwanjani Wembley dhidi ya Barcelona Jumamosi na hakuweza kusafiri kwenda Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa mwisho dhidi ya Mainz siku moja baadaye.
Alipotakiwa kusema neno moja tu juu ya uwezekano wa kuwapo kwa nyota huyo wa kimataifa wa Englanda katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu, Klopp alisema: "Sijui.!"
Baada ya kuifunga Barcelona mabao 4-0, baada ya siku moja Liverpool ilijikuta ikifungwa idadi kama hiyo ya mabao na Mainz ambayo iliwahi kufundishwa na Klopp.
Hata hivyo, Klopp amesema timu yake iko katika njia sahihi baada ya kucheza michezo tisa ya kirafiki katika maandalizi ya msimu.
"Kila siku niko tayari," alisema. "Tumecheza michezo mingine tukiwa vizuri kwelikweli, mengine tukiwa wachovu kidogo.
"Kwa uhakika tutakuwa vizuri kwa ajili ya mchezo wa kwanza wiki ijayo. Lakini kama Arsenal itakuwa msimu bora dhidi yetu, kutakuwa na makosa sehemu katika msimu.
"Tunatakiwa kusonga mbele. Huu ni mchezo wa kwanza tu. Hatuwezi kufanya uamuzi wa msimu mzima kwa mchezo mmoja.
"Lakini tunahitaji kuwa bora iwezekanavyo. Na hivyo ndivyo tutakavyokuwa kwa asilimia 100."
Post a Comment