0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO ametetea uamuzi wake aliouchukua juu ya kiungo Bastian Schweinsteiger pamoja na kupondwa sana na wapinzani wake.
Schweinsteiger, 32, ameonekana kutokuwa sehemu ya mipango ya Mourinho uwanjani Old Trafford ambaye ameripotiwa akisema kwamba mchezaji huyo atafanya mazoezi na wachezaji wa akiba.
Umoja wa wanachama wa wachezaji bora wa Ulaya, (FifPro) ulikaririwa ukisema kocha Mourinho anapaswa kufungwa jela kwa jinsi alivyomtendea Schweinsteiger ndani ya Manchester United, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Munich, Karl –Heinz Rumamenigge aliishambulia klabu hiyo ya Ligi Kuu.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa Mourinho alisema: "Kilichotokea ni kile kinachotokea katika kila klabu duniani. Kwamba kocha anachagua kikosi chake na anachagua baadhi ya wachezaji kwa ajili ya msimu, ni hilo tu.
"Kwa kawaida napenda kufanya kazi na wachezaji 20 ukijumlisha na makipa watatu, kitu ambacho nimekuwa nikikifanya kwa takribani miaka 15. Lakini tunao wachezaji wengi, mashindano mengi, hasa Europa League, ambayo hubadirisha kwa kiasi kikubwa msimu.
"Unakuwa katika hatari kubwa unaposafiri sana, kucheza Ligi Kuu. Kwa hiyo nilifanya uamuzi wa kuwa na wachezaji 23 na makipa wawili, ambao wanatosha. Ninapaswa kufanya uamuzi, ni rahisi."
Schweinsteiger aliondoka Bayern na kujiunga na United msimu wa majira ya joto mwaka jana  alianza katika michezo13 ya Ligi Kuu katika msimu wa 2015-16 chini ya bosi wa zamani Louis van Gaal.

Mourinho amekiri  kuwa na wasiwasi kwa kukosa maandalizi ya kutosha kufuatia ziara ngumu ya maandalizi ya China ambayo ilishuhudiwa kuahirishwa kwa mchezo ‘derby’ ya Manchester jijini Beijing.
Lakini aliahidi kubadilisha staili ya mrithi wake Louis van Gaal.
Wakati wangu ni tofauti na wa Mr Van Gaal,” aliongeza.
“Nataka kuweka hili sawa kwamba sisemi kwamba timu yangu ni bora au ina mawazo mazuri, siyo hivyo kabisa. Timu yangu ni tofayti nay a Mr Van Gaal.
“ Ni hatua ngumu kubadili mwenendo.  Inaweza kuwa rahisi kwangu kuwa na wachezaji 20 wapya na kuanza kuanzia ziro. Kwa miaka miwili watafuata kanuni ileile ya uchezaji  ambayo siyo yangu moja kwa moja.
“Bila ya kupoteza utambulisho, wachezaji kila siku watajaribu kuiga kile kocha anachokitaka. Baada ya miaka miwili kutakuwa na kitu katika akili zao ambacho kitakuwa vigumu kubadilika.
Katika mkutano huo, Mourinho alizungumzia mchezo wa Ngao ya Jamii  wa Jumapili  dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu, Leicester City.
Kocha huyo alisema mchezo huo wa ufunguzi wa msimu unaweza kuwa na maana kubwa isiyokuwa ya kawaida kufuatia kuvurugika kwa ziara ya msimu ya China.
"Kila kitu ni muhimu. Maandalizi ya msimu wetu ulikuwa wa maajabu. Ulikuwa mzuri kwa baadhi ya wachezaji na kwa wengine hakutosha. Idadi ya michezo haikutosha," alisema.
"Mechi ambao hatukucheza dhidi ya City haukuwa mzuri kweli. Wiki ambayo hatukucheza tulipokuwa China haikuwa nzuri kwetu. Tulihitaji kufanya mazoezi, tulihitaji kucheza. Tulihitaji kufanya mazoezi dhidi ya timu nyingine kama tulivyofanya dhidi ya Everton na Galatasaray.

"Sasa wiki hii tuna mchezo mwingine wa mazoezi. Kwa wachezaji ambao walikuwapo msimu uliopita utakuwa na maana. Walishinda Kombe la FA. Tunapaswa tucheze.
"Tuna mabadiliko sita, siyo matatu. Hivyo nitawapa muda baadhi ya wachezaji, kwa sababu hawana uwezo wa kucheza dakika 90."

Post a Comment

 
Top