MUNICH, UJERUMANI
KARL-HEINZ RUMMENIGGE ambaye ni
Mkurungezi Mtendaji wa Bayern Munich ameikosoa Manchester United kwa kumshusha Bastian
Schweinsteiger hadi katika wachezaji wasiocheza reserves.Schweinsteiger (pichani juu) ambaye amefikisha miaka 32 Jumatatu, ameamriwa kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa kikosi cha Manchester United cha U-23 baada ya kuambiwa na kocha Jose Mourinho kwamba hayumo kwenye mipango yake.
"Ilinipa wakati mgumu kuamini baada ya kusoma habari hiyo," Rummenigge alisema kwenye mkutano wa waandishi wa habari Jumatano. "Hii haijawahi kutokea Bayern Munich na haitatokea."
... Rummenigge
Schweinsteiger aliondoka Bayern na
kujiunga na United msimu wa uliopita katika usajili wa majira ya joto na
ameanza katika michezo 13 ya Ligi Kuu England
katika msimu wa 2015-16.Rummenigge aliongeza: "Mbele ya safari wachezaji watafikiria mara mbili kujiunga na klabu ya aina hii (United), ambazo zinaweza kumpandisha thamani zaidi zinapomtaka mchezaji kuliko klabu za Borussia Dortmund au Bayern Munich za Ligi ya Bundesliga zingeweza kufanya.
"Inaonekana hii ni kama kiasi ambacho wachezaji wanapaswa kulipa kama watajiunga na klabu kama hizi."
Kocha wa zamani wa Bayern, Ottmar Hitzfeld alisema kitendo alichofanyiwa Schweinsteiger ni hali ya kutoonesha heshima na aliongeza: "Nji hii ni ngeni kwangu."
Kiungo wa United amecheza jumla ya michezo 31 chini ya kocha wa zamani Louis van Gaal msimu wa 2015-16, huku akiwa majeraha ya goti yakimuweka nje kwa miezi kadhaa.
"
Ni ukosefu wa heshima kwa mchezaji mwenye thamani kubwa. Ni njia ambayo
imenishangaza sana. Schweinsteiger ni mchezaji muhimu, bingwa wa Kombe la Dunia,
ana hadhi, wakati huo huo ni mtu mwenye tabia njema sana, hakustahili kutendewa
hayo” alisema Hitzf.
Hii
ni mara ya pili kwa Schweinsteiger kufanyiwa hivyo, mara ya kwanza ikiwa ni
mwaka 2005 wakati kocha wa Bayern wa wakati huo, Felix Magath alipomlazimisha
kufanya mazoezi na wachezaji wa akiba kwa madai kwamba hakuwa na nafasi katika
kikosi chake cha kwanza.
Hata
hivyo, Schweinsteiger aliibuka na kufanya mambo makubwa na kurudi katika kikosi
cha kwanza, kuanzia hapo akatwaa mataji manane ya Bundesliga, saba ya Kombe la
DFB-Pokals na mwaka 2013 alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya
kuichapa Borussia Dortmund 2-1 katika dimba la Wembley.
... Mourinho
Kocha
wa zamani wa United, Louis van Gaal alitoa Pauni 10 milioni na kiungo huyo
alikuwamo katika kikosi kilichotwaa taji
la FA Mei mwaka jana kwa kuichapa Crystal Palace 2-1.
Wakati huohuo, Kocha wa Bayern Carlo
Ancelotti ametupilia mbaloi madai kwamba kiungo huyo atarudi Allianz Arena."Schweinsteiger siyo sehemu ya mawazo yetu. Sidhani kama huu ni muda wa kurudi Bayern Munich," Ancelotti aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.
Hata hivyo, Rummenigge alisema anaweza kufikiria Schweinsteiger kurudi Bayern katika siku zijazo lakini siyo kwa majukumu ya kucheza.
Post a Comment