0


MANCHESTER, ENGLAND
PAUL POGBA (akiwa akiwa ndani ya gari) ametua England tayari kuvunja rekodi ya uhamisho wa dunia wa Pauni 110 milioni kutoka Juventus na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United. 

Kurudi Old Trafford  kwa kiungo huyo Mfaransa imekuwa habari kubwa  iliyochukua muda mrefu katika usajili wa majira haya ya joto lakini sasa anakaribia kumaliza akiwa anaendeshwa kupelekwa katika viwanja vya mazoezi vya United vya  Aon Training Complex  akiwa ndani ya gari aina ya  Chevrolet Camaro  Jumatatu mchana  kwa ajili ya kwenda kupimwa vipimo vya afya baada ya kutua na ndege akitokea jijini Nice kwa safari aliyoianzia New York. 

Pogba anarudi United – klabu iiliyomuacha kwa fidia ya Pauni 800,000  mwaka 2012 – kwa ada ya rekodi ya dunia.
Viwanja vya mazoezi vya United tayari vina vifaa kwa ajili ya vipimo vya afya ya Pogba.

United ilithibitisha Jumapili kwamba Juventus imewaruhusu kumfanyia vipimo Pogba.  
Hiyo inamaanisha  Pogba atakuwa mchezaji ghari zaidi duniani. United ikimchukua kwa kiasi kikubwa zaidi ya kile Real Madrid  ilichotoa kumchukua Gareth Bala mwaka 2013  Pauni 85 milioni kutoka Tottenham.

...ndege aliyotua nayo.
Uchukuaji wa vipimo vya afya kwa Pogba ni kama wajibu tu, huku United ikitarajia kumsaini rasmi staa huyo kati ya Jumanne na Jumatano wiki hii.


Pogba mwenye umri wa miaka 23, alitua Uwanja wa Ndege wa Manchester Jumatatu asubuhi akitokea New York alikokuwa kwenye mapumziko. 
Akaunti ya Twitter ya Uwanja wa ndege wa  Manchester ilidokeza katika ujio wake kwa kuposti gave picha ya ndege binafsi ikitua.
Picha hiyo ilikuwa na maelezo  'abiria muhimu ndio kwanza ametua uwanja wa ndege. Kuna mtu yeyote anayeweza kukisia atakuwa ni nani?
Pogba aliondoka United na kujiunga na Juventus mwaka  2012 alikuwa amecheza michezo saba tu ya timu ya wakubwa katika michezo yote ya Ligi Kuu, mengine yote akiwa benchi.
Alikwenda kuisaidia Juventus kushinda mataji manne ya Ligi ya Serie, Makombe mawili Coppa Italia na  kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2014-15.
Pia, alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichomaliza katika nafasi ya pili ya Euro 2016.

Post a Comment

 
Top