LONDON,
ENGLAND
ANTONIO
CONTE (pichani juu) anaweza kuwa kocha wa kwanza kutimuliwa katika Ligi Kuu England kati ya
makocha sita wanaoanza vita ya ligi hiyo Jumamosi.
Ligi Kuu England itakuwa na vita kubwa
msimu huu kutokana na kuwahusisha makocha bora duniani kuanzia Jose Mourinho, Arsene Wenger,
Pep Guardiola, Jurgen Klopp, Conte na Claudio Ranieri.
Guardiola
Kocha Guardiola amewasili kuinoa Manchester
City wakati Jose Mourinho ameanza kazi Manchester United.Presha ipo pia kwa Arsene Wenger kufika mwisho wa kileleni kutokana na changamoto iliyopo, wakati Klopp wa Liverpool na Maurcio Pochettino wa Tottenham wanatarajiwa kuziimarisha timu zao.
Mourinho
Lakini kocha wa Chelsea, Conte anafikiriwa
kuwa atashindwa kuwa na mafanikio kutokana na mwajiri wake.Kocha Conte ametakiwa na Bilionea anayemiliki klabu hiyo, Roman Abramovich akipewa kibarua cha kuirudisha timu hiyo kwenye ushindi baada ya kupotea katika ushindani msimu uliopita.
Mpaka sasa, Conte amesajili wachezaji wawili lakini kujiamini kwake na mbinu zake zitasababisha athari Stamford Bridge.
Wenger
Lakini inaaminika atakuwa wa kwanza
kupoteza kibarua chake kati ya makocha sita wakubwa waliopo Ligi Kuu msimu huu.Conte amepewa wastani wa 7/2 akifuatiwa na, Klopp, Wenger, Mourinho, Guardiola na Pochettino kuondoka katika klabu zao.
Waliopiga kura wanahofia Conte atakuwa akilengwa na mikono ya Abramovich labda kama Chelsea itaanza msimu kwa kasi.
Bosi wa Liverpool Klopp na kocha mpya wa Old Trafford, Mourinho watafuata wakiwa na wastani 4/1 – na kocha wa Arsenal Wenger, Pochettino na Guardiola wakiwa na wastani wa 5/1.
Post a Comment