0


KINSHASA, CONGO
KUTOKA mahabusu ya Nairobi hadi katika jela ya Kinshasa. Mwanamuziki mkongwe wa Muziki wa Rumba  ameachiwa kwa dhamana.
Koffi alikamatwa nyumbani kwake  jijini Kinshasa, Congo wiki iliyopita baada ya kumshambilia  mnenguaji wake wa kike  walipokuwa ziarani Kenya na kuhukumiwa kwenda jela miezi 18.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 59, alitolewa kwa dhamana Jumamosu usiku, baada ya kukaa kizuizini siku nne katika Gereza la Makala.
Mmoja wa mwanasheria wake Benoit Tayeye alifafanua sababu za mwanamuziki huyo kupewa dhamana.
 “Kwanza anaishi katika makazi yanayofahamika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni maarufu na mali zake nyingi zipo nchini,” alisema Tayeye.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, madai ya kushambulia dhidi yake bado hayajafikishwa mahakamani pamoja na kwamba ameachiwa kutoka Gereza la Makala lililopo jijini Kinshasa.

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake kamili ni, Antoine Agbepa Mumba Olomide, alikamatwa mara mbili ndani ya wiki, baada ya mara ya kwanza alikamatwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa sababu ya kumpiga teke mcheza shoo wake wa kike tumboni walipokuwa wakiwasili uwanja wa ndege kwa ajili ya kufanya onesho la muziki.
Kutokana na tukio hilo alikamatwa na kulazwa mahabusu kwa usiku mmoja kabla ya kurudishwa Congo.
Awali Olomide alikanusha kuwapo kwa tukio hilo ambalo lilikuwa limenaswa kupitia kamera, lakini baadaye aliomba radhi kwenye runinga ya Congo na kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook.

Post a Comment

 
Top