0


LIVERPOOL, ENGLAND
AC MILAN hamtaki. Besiktas hamtaki. Ajax inaweza kumchukua kama atapunguza mshahawa wake.
Straika wa Italia mwenye umri wa miaka 25, kwa sasa anapokea  mshahara wa Pauni 90,000-kwa wiki akiwa Liverpool na miamba hiyo inahofia kumuweka kwenye mipango yake.
Balotelli amefunga mabao mawili katika Ligi Kuu tangu Aprili 2014 na kwa hatua hiyo uwezo wake unaweza kuwa umemtia doa kwa klabu kadhaa.
Kitendo cha kuvuta sigara hadharani kinaongeza wasiwasi kwa uwezo wa straika huyo.

Akiwa amekaa katia Hoteli ya Strainer katika Kijiji cha Italia cha Portofino, Kusini mwa Genoa, Balotelli anaonekana kama hana jukumu lolote linalomtaka kuwa mwangalifu duniani.
Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan mapema alipana boto na marafiki zake kwa ajili ya safari hiyo.
Hiyo ni licha ya kwaamba straika huyo kuambiwa hatabaki tena Liverpool.

Wakati Kocha Jurgen Klopp na watu wengine kwenye timu wakisafiri kwenda Marekani kwa ajili ya ziara ya mwanzo mwa msimu, Balotelli ameachwa akitakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha chini ya maika 21.
Hii sio mara ya kwanza kwa Balotelli kunaswa akivuta sigara – alibambwa katika klabu jijini Manchester na  katika baa moja mjini Miami.

Klabu ya Ajax ndio pekee iliyoonesha nia ya kumtaka Muitaliano huyo lakini kuna tofauti kubwa kati ya mshahara wake na ule uliopo kwenye muuondo wa klabu hiyo.
Miamba hiyo ya  Amsterdam haiwezi kulipa mshahara zaidi ya Pauni 40,000-kwa wiki, ambao ni nusu zaidi ya ule Balotelli anaoupata Liverpool.

... akiwa na kikosi cha U-21
Awali, AC Milan, Inter Milan, Sampdoria na  Besiktas zilikuwa zikihusishwa na straika huyo lakini hakuna hata klabu moja kwa sasa inayovutiwa na gharama yake.
Wakala bora kabisa, Mino Raiola anaendelea kufanya kazi ya kumtafutia dili mteja wake.
Balotelli  amebakisha miezi 12 katika mkataba wake na Liverpool ingependa kurudisha sehemu ya Pauni 16 milioni ilizotumia kumnunua mwaka 2014.

Post a Comment

 
Top