0


                        
                           MANCHESTER, ENGLAND
CLAUDIO BRAVO yuko njiani kwenda Manchester kumalizia uhamisho wake wa Pauni 14.5 milioni kujiunga na Man City.
Kocha Pep Guardiola alimtaja kipa huyo wa  Barcelona kwamba ndiye anayemhitaji Etihad ili kuwa kipa namba moja msimu huu.
City imeshakubaliana maslahi binafsi na kipa huyo wa kimataifa wa Chile wiki iliyopita lakini Barca ilikuwa ikisita kumwachia kabla ya kuwa na uhakika wa kupata mbadala wake.

Bravo akipangu penalti
Bravo, 33, amecheza katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya La Liga dhidi ya Real Betis Jumamosi na miamba hiyo ya Catalunya inaamini kwamba sasa inaweza kumsajili kipa wa  Ajax, Jasper Cillessen.

           kipa anayechukua nafasi ya Bravo, Barcelona
Na nyota huyo wa zamani wa Real Sociedad alionekana Barcelona Jumanne asubuhi.
Inafahamaika kwamba City will itathibitisha kuingia dili- ambalo linaweza kupanda hadi Pauni 18 milioni- Jumatano baada ya kuridhika na vipimo.
Kuwasili kwa Bravo ni dhahiri kunathibisha kumaliza enzi za kipa namba moja wa City, Joe Hart aliyedumu na klabu hiyo kwa miaka 10.

Kocha Guardiola aliyemchinjia Hart baharini.
Kocha Guardiola tayari ameshaamwacha  kipa huyo namba moja wa England katika kikosi chake cha kwanza na kumpa nafasi kipa, Willy Caballero.
Na Bravo atachukua nafasi kwa kuwa kipa chaguo la kwanza – hivyo basi kumshusha zaidi Hart even katika mpangilio wa makipa.
Hart mwenye umri wa miaka 29- atalazimika kuondoka City ili kuokoa nafasi yake ya kipa namba moja England ikiwa chini ya bosi mpya, Sam Allardyce ambaye akiri kwamba itakuwa vigumu kumchagua kama atakua akiendelea kukaa benchi.

Post a Comment

 
Top