0


MILAN, ITALIA
JOSE MOURINHO amedaiwa kukutana na Mario Balotelli kwa lengo la kumpa straika huyo wa Liverpool ushauri wa jinsi anavyoweza kumudu kurudi katika kiwango chake.

Kocha wa Liverpool, Klopp
Habari kutoka Italia zinasema wawili hao ambao wameshawahi kufanya kazi, kwa kipindi kifupi Inter Milan, walikutana katika mkutano rasmi, siku chache zilizopita.
Inadaiwa Mourinho alimwambia Balotelli ni lazima abadili tabia zakekama anataka kupata mafanikio na hatimaye aliutambua uwezo wake.
Akiwa na umri wa miaka 26, straika huyo wa kimataifa wa Italia, ameshazitumikia Inter na AC Milan, pamoja na Manchester City na klabu yake ya sasa Liverpool, ambao kwa sasa hawamhitaji Anfield.

Balotelli
Kiti cha kushangaza, katika mkutano huo, Mourinho hakutoa ushari wa kumtaka Balotelli kujiunga na Manchester United.
Balotelli, alijiunga na Liverpool mwaka 2014 kwa Pauni 16 milioni, hatakiwi klabuni hapo na Kocha Jurgen Klopp na Mjerumani huyo anataka kumuondoa kabla ya kufungwa kwa dirisha la majira ya joto wiki mbili zijazo.

Mourinho
Fowadi huyo  msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo AC Milan lakini Rossoneri ilikataa kumchukua  moja kwa moja.
Amerudi Melwood mapema katika majira ya joto na kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya akiwa na Liverpool lakini hana muda mrefu Merseyside.

Post a Comment

 
Top