0


LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA amesisitza kwamba hatendewi haki na waamuzi na wachezaji wengine katika Ligi Kuu England.
Straika huyo wa Chelsea alifunga  bao la ushindi katika dakika za mwisho dhidi ya West Ham Jumatatu usiku lakini ilikuwa apewe kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya kipa wa Adrian.
Costa  ambaye hivi karibuni alihusishwa kutaka kurudi katika klabu yake ya Altetico Madrid ya Hispania alionyeshwa kadi 11 msimu uliopita, alipata kadi ya njano katika dakika ya 19 katika mchezo huo wa ufunguzi uwanjani Stamford Bridge.
Lakini pamoja na ushahidi, he anaamini kwamba waamuzi na wapinzani wake wanamuwinda.
Alisema: “Nitakuwa mwaminifu, ninawindwa na waamuzi hapa. Kama ninafanya tukio fulani, kwa kiasi kikubwa ni tofauti kama mchezaji mwingine atafanya hivyo.

"Nahitaji kuangaliwa, watu hawa wananiwinda.
"Ni kitu fulani ambacho ninatakiwa kudili nacho na ninamuomba Mungu kwamba hivi vitu visinisumbie na kuchukua mlolongo katika michezo yangu, ambayo inaweza kutokea wakati mwingine na kupewa kusimamishwa.
“Nafahamu kuhusu sheria mpya (Sheria mpya ya kupewa kadi ya njano kwa kubishana sana). Mara ya pili nilipokwenda kuzungumza naye alinionyesha kadi ya njano. Ingawa sijaikubali lakini nimeelewa. Nilienda kumuomba msamaha wakati wa mapumziko na yakaisha,” alidai Costa.

Hata hivyo, kocha wa West Ham, Slaven Bilic alidai kwamba Costa hakucheza rafu hiyo kwa makusudi ingawa alistahili kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano kwa kuchelewa kuweka mguu wake kwa kipa wake.

“Nimelitazama tukio lile tena, sidhani kama ilikuwa rafu ya hatari. Kwa mtazamo wangu haikuwa bahati mbaya lakini alichelewa. Mara tisa kati ya 10 ukiona rafu kama ile mchezaji anapata kadi ya njano,” alisema Bilic.
Septemba mwaka jana, Costa alitembeza ubabe kwa walinzi wa Arsenal, Gabriel na Laurent Koscielny huku Gabriel akipewa kadi nyekundu katika pambano hilo ingawa Costa alimchapa makofi Koscielny na hakuonyeshwa kadi yoyote na mwamuzi.
Machi mwaka huu katika pambano la robo fainali za FA dhidi ya Everton, Costa alipewa kadi yake nyekundu ya kwanza katika soka la Kiingereza baada ya kugombana na kiungo wa Everton, Gareth Barry. 

Picha za awali za kamera zilionyesha Costa akimuuza Barry baada ya kusuguana vichwa.
Kabla ya hapo Costa alikuwa ametema mate upande wa kumwelekea mwamuzi baada ya kuonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi huyo kwa kosa la kugombana na huyo huyo Barry. Costa alifungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Pauni 20,000.

Mei 2 mwaka huu katika sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham ambayo uiliinyima Tottenham ubingwa katika dimba la Stamford Bridge, Costa alichomwa vidole jichoni na kiungo wa Tottenham, Moussa Dembele na kuachwa jicho lake likiwa jekundu. Dembele alifungiwa mechi sita kwa kosa hilo na mpaka sasa hajaanza kucheza katika mechi za Ligi Kuu England.

Post a Comment

 
Top