MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO amemwambia kiungo, Bastian Schweinsteiger (pichani juu) asahau kuitumikia tena Manchester United.
Pamoja na kuwekwa kando na Mourinho na
kutakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha
akiba, Schweinsteiger haonyeshi dalili za kutaka kuondoka akiwa
amebakisha miaka miwili katika dili linalomlipa Pauni 160,000- kwa wiki .
Hivi karibuni, kiungo Schweinsteiger alisisitiza kwamba hatajiunga na klabu nyingine ya Ulaya baada Kocha Mourinho kumtoa kwenye mipango yake ya baadaye.
Hivi karibuni, kiungo Schweinsteiger alisisitiza kwamba hatajiunga na klabu nyingine ya Ulaya baada Kocha Mourinho kumtoa kwenye mipango yake ya baadaye.
Kiungo huyo wa Kijerumani alishinda Kombe la Dunia amekataa kujiunga na klabu nyingine ya Ulaya
na kuichia United ipiganie kumuuza kabla ya siku ya mwisho ya usajili.
Katika kupigilia msumari wa mwisho, Mourinho amesema ni heri
amtumie kijana wa kikosi cha academy
kuliko kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 katika kikosi cha kwanza kama
kutakuwa na upungufu.
“Nina wachezaji 23 katika kikosi changu na kwa utaratibu hakuna atakayeondoka, kwa sababu sitaki yeyote aondoke,” alisema Mourinho.
“Hakuna atakayeingia na wachezaji 23 wanatosha sana. “Kama tutakuwa na aina yoyote ya tatizo la nafasi, nina wachezaji vijana wachache katika academy, itakuwa zaidi ya furaha kuongeza kasi katika mchakatokwa kuwaingiza katika kikosi kwa mara nyingine.”
... Schweinsteiger akiwa na Kombe la Dunia.
Alipoulizwa kama Schweinsteiger anaweza
tena kuitumikia United, Mourinho alisema: “Nadhani ni jambo gumu kutokea. Sijasema
haiwezekani, nasema ni vigumu kwa sababu tumeshafanya uamuzi kuhusu Pogba (Paul), Herrera (Ander),
Schneiderlin (Morgan), Fellaini (Marouane) na Carrick (Michael), tuna wachezaji watano
katika nafasi mbili, kwa hiyo ni vigumu kwa nafasi hiyo kutokea.“Siwezi kumjibia maswali yake. Ni kuhusu maisha yake, kazi yake, ana mkataba na Man United. Ana haki ya kufanya maamuzi hayo na kukaa, hilo sio tatizo kwetu.
“Soka limejengwa kwa kufanya maamuzi. Nimefanya hivyo katika kazi zangu siku zote. Sio kwa ajili yangu, kila mmoja anafanya, lakini baadhi ya wachezaji wanachukulia katika mtazamo tofauti.
“Kwa kweli, Bastian siyo mzungumzaji sana. Ametoa kauli yake ya mwisho ambayo ana haki ya kuitoa, kama alivyofanya. Nilifikiria pindi niliposoma baadhi ya maneno ya watu wa Bayern Munich, wangeweza kukimbilia Manchester na kumrudisha, lakini hapana, hilo halitatokea.
“Ninashangazwa Karl-Heinze Rummennigge hayupo hapa kumrudisha. Kwa hiyo ninadhani tuna wiki tulivu, hatukuzungukwa na helikopta, kumsubiri mtu kuondoka au kuwasili, kwa hiyo nina zaidi ya furaha na kikosi ambacho ninacho.”
Kuhusu
ratiba ta Europa League , Mourinho alisema: “Ni nzuri kwa upande wetu kwa
sababu tunadhani tupo kwenye Ligi ya Mabingwa. Tunajua ni kundi gumu, lakini
nadhani ni zuri, kwa sababu kama unakutana na timu zisizojiweza, hata mashabiki
hawatafurahia usiku wa Alhamisi uwanjani Old Trafford, kwa hiyo ninadhani ni
vizuri kwa mashabiki na wachezaji, kwa sababu tutapata hamasa zaidi.”
Post a Comment