MADRID,
HISPANIA
FERNANDO
TORRES amejibu mapigo kwa klabu yake ya zamani ya Liverpool baada ya kuitwa
msaliti kufuatia kuhama na kujiunga na Chelsea mwaka 2011.
Uhamisho wa Mhispania
huyo ulisababisha hasira kwa mashabiki wa Liverpool baada ya kujiunga na wapinzani
wao katika Ligi Kuu kwa ada ya Pauni 50 milioni, na kuweka rekodi ya uhamisho Uingereza.
Lakini
Torres mwenye umri wa miaka 32, amefunguka kuhusu kujiunga kwake na Chelsea, ambako
alishinda Kombe la FA na taji la Ligi ya Mabingwa, kwa kudai kwamba hakuwa na
chaguo lingine zaidi ya kuondoka
Liverpool.
Kwa mujibu
wa kitabu cha Ring of Fire, kinachozungumzia
historia ya mchezaji huyo, Torres alisema: “(Mkurugenzi wa Michezo
Damien) Comolli aliniambia kwamba wamiliki wapya (Fenway Sports Group), wana
mawazo mapya juu ya kuendesha uwekezaji wao.
... akiwa Liverpool
“Wanataka
kuleta wachezaji vijana, kutengeneza kitu kipya. Nikajifikiria, hii itachukua
muda mrefu sana kufanya kazi. Labda miaka miwili, mitatu, minne, labda miaka 10.
“Sikuwa na
muda huo. Nilikuwa na umri wa miaka 27. Sikuwa
na muda wa kusubiri. Nilihitaji kushinda. Mpaka sasa tuna miaka mitano bado
wanajaribu kujijenga- wakiendelea kushika karibu katika nafasi ileile katika
ligi tangu nilipoondoka.”
....akiwa Chelsea
Straika huyo
ambaye sasa amerudi Atletico Madrid- klabu ambayo ilitengeneza jina lake – pia alidai
kwamba alikuwa kama mtu eliyeumbwa kwa ajili ya kubeba makosa ya timu hiyo.
“Iliwasilishwa
kama nilikuwa msaliti. Haikuwa hivyo katika majadiliano.
... akiwa Altetico Madrid
“Liverpool
haikukubali kwamba ilifanya kitu kibaya kwa timu nzima. Walitaka kumtafuta mkosaji
mmoja.”
Torres ambaye baadaye aliuzwa na Chelsea kwenda AC Milan alipachika
mabao 65 katika michezo 102 ya Ligi
Kuu akiwa na Liverpool, na alichaguliwa
katika timu ya wachezaji bora wa mwaka wa kulipwa (PFA) na kikosi cha dunia FIFPro katika misimu
miwili ya mafanikio.
Post a Comment