MANCHESTER,
ENGLAND
JOSE
MOURINHO ameonywa na kutakiwa kuwa makini na straika wake, Zlatan Ibrahimovic
kwani anaweza kusababisha matatizo makubwa ndani ya Old Trafford.
Inadaiwa
kwamba Ibrahimovic ni mtata kama hatapangwa kuwa straika namba moja ndani ya
kikosi cha Manchester United.
Hayo yamesemwa na mchezaji wa zamani
wa kimataifa wa Sweden ambaye pia aliwahi kucheza timu moja na straika huyo, Pontus
Kamark.
Kamark
Pamoja na kutoa taadhari hiyo,
Kamark ambaye pia aliwahi kuichezea Leicester katika Ligi Kuu England miaka ya 1990s,
anaamini Ibrahimovic ni mchezaji mzuri kwa United.Kamark amekwenda mbali zaidi na kudai mchezaji huyo wa zamani wa PSG anaweza kuwa na manufaa kama ilivyokuwa kwa staa wa zamani wa United, Eric Cantona.
Lakini Kamark ana hofu kwamba Ibrahimovic anaweza kuzalisha matatizo kama ilivyokuwa Barcelona kama hatawekwa mstari wa mbele katika safu ya ushambuliaji.
Kamark, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka nyumbani kwao, alisema: "Amejiingiza katika kila hoja.
Ibrahimovic akiinua ngao
Alimwita hata Pep Guardiola mwanafalsafa kwa sababu Messi alitishwa na ubora wake na Zlatan hakutaka kuwa No.2.
"Kama watu wataingia kwenye anga zake anaweza kuwapiga. Anaweza kukuangusha mazoezini. Anaweza kufanya chochote ili akae kwenye kiti cha enzi. Anaweza kufanya kwa njia nzuri au mbaya – hususan kama mtu hamkubali kuwa yeye ni Namba 1.
"Siku zote amekuwa akitafuta sababu, kwa kuwa hataki kuwa namba No.2 - Zlatan anataka kuwa No. 1."
Ibrahimovic na Marcus Rashford
Ibrhimovic, ambaye aliipa taji United
kwa kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester katika mchezo wa
Ngao ya Jamii, ameshasema anaamini nahodha wa Mashetani Wekundu, Wayne Rooney ni
patna wake sahihi.Na Kamark alisema anaamini wawili hao wanaweza kufanya vizuri- lakini akaonya matatizo yanayoweza kutokea kama hawatakuwa na mshikamano.
Rooney
Kamark aliongeza: "Natumaini
watadumu, yeye na Rooney- na itakuwa hivyo, nadhani watakuwa na kombenesheni
bora."Kama hawataenda sawa, (Ibra) ataanza kuunda matatizo. "Unaweza kuwa na pande zote mbili za Zlatan. Huwa anachukua nafasi kubwa mno, anaweza kusababisha matatizo mengi lakini anaweza pia kuyafanya mambo yakawa magumu bila ya uwepo wake."
Post a Comment