0



MADRID, HISPANIA
MARTIN ODEGAARD kinda mwenye umri wa miaka 17 amewagombanisha kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na Rais wa klabu, Florentino Perez.
Kisa kinadaiwa kuwa Zidane hakutaka kuambatana na kinda huyo anayecheza nafasi ya kiungo katika safari ya maandalizi ya msimu, Canada lakini Perez amelazkimisha Odegaard awemo.
Hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kutokubaliana tangu Zidane alipochukua kibarua cha kuinoa Real Madrid Januari.
Rais Perez anataka Odegaard awemo kwenye kikosi cha kwanza katika ziara hiyo kwa sababu imo kwenye mkataba wake na kwa sababu uwepo wake unaweza kuisaidia Madrid kumpatia klabu Marekani ya Kaskazini katika usajili wa majira haya ya joto.


Odegaard akichukua begi lake katika basi baada ya  Real Madrid kuwasili jijini Montrea.

Lakini  Zidane ambaye alikubali kijana huyo atolewe kwa mkopo msimu huu, amepinga kuambatana naye kwa kuwa hana mipango ya kumtumia kwenye kikosi cha kwanza.
Zidane aliyevurugana na Rais Perez kuhusiana na Odegaard.
Gazeti la Le10Sport la Ufaransa lilikwenda mbali zaidi baada ya kudai kuwa Perez alilazimisha Odegaard awepo kwenye ziara hiyo, na likadai kwamba mkongwe huyo wa Ufaransa (Zidane) hakuwa na furaha na kuhisi kuingiliwa katika majukumu yake.
Klabu ya Hamburg ya Ujerumani imeonyesha nia ya kumchukua Odegaard katika Ligi ya Bundesliga msimu ujao na Liverpool – ambayo awali aliikataa na kuichagua Madrid – nayo pia imehusishwa naye. 



              Odegaard alijiunga Real Madrid Januari 2015.


Lakini Real Madrid inataka kumpeleka mchezaji huyo katika klabu nyingine ya Hispania na inataka kumpa mchezo mmoja wa kirafiki wa maandilizi ya msimu.
Pia inadaiwa Real Madrid inataka kwenda na Odegaard katika mchezo wa fainali ya Super Cup Agosti 9, kwa sababu mchezo huo utachezwa katika nchi yake ya Norway.

Odegaard akiwa katika pozi la picha na Cristiano Ronaldo na  Sergio Ramos mwaka 2015.


Real Madrid ilimsaini Odegaard Januari 2015 lakini ilitegemea angeweza kuwa na mafanikio ya haraka na kuingia katika kikosi cha kwanza lakini amekuwa na maendeleo hafifu katika kikosi B cha 'Castilla’ ambacho awali kilikuwa kikifundishwa na Zidane. 
Hii siyo mara ya kwanza kwa Zidane kutibuana na Odegaard. Wakati alipokuwa akifundisha Castilla, Mnorway huyo alikuwa akikosekana mara kwa mara mazoezini kwa sababu alikuwa akihudhuria  mazoezi ya kikosi cha kwanza, wakati huo kikiwa chini ya Kocha Carlo Ancelotti.
Kocha Ancelotti hivi karibuni alikiriwa akdia kwamba hakuwahi kuomba Odegaard asajiliwe na alilazimishwa kumbeba pale ilipowezekana.

Marcelo, Casemiro na Danilo (kulia kwenda kushoto ) safarini  Canada


Ancelotti alimpa nafasi Odegaard katika mchezo wa mwisho wa msimu wa 2014-15 kabla kocha huyo hajatimuliwa.
Kocha Zidane anafahamika kwa kukuza vijana Real Madrid lakini anadhani kinda kiungo mkabaji, Marcos Llorente na kinda mwingine kiungo mshambuliaji, Marco Asensio, ambao wote wako safarini  jijini Montreal na kikosi hicho, wako vizuri zaidi ya Odegaard. 

Karim Benzema akiwa safarini
Watoto wawili wa Zidane, Luca na Enzo, wote wako na kikosi hicho Canada, ambacho kinawakosa baadhi ya nyota walioshiriki Euro 2016. 

Post a Comment

 
Top