OHIO, MAREKANI
ZINADINE ZIDANE amesema Real Madrid
haijakata tamaa katika kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba (pichani juu) katika usajili
huu wa majira ya joto.Kocha huyo wa Real Madrid alifunguka kwamba chochote kinaweza kutokea kabla ya siku ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Manchester United inaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumasajili Pogba, 23, ingawaje chanzo cha ndani ya Juventus kimesema timu hiyo haiwezi kukubali dau la chini ya Euro 120 milion kwa ajili ya kumtoa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa na imeitaka Manchester United kulipa ada ya Euro 25 milioni kwa ajili ya wakala wa Pogba, Mino Raiola, na uongozi wa Old Trafford unasita kukidhi mahitaji hayo.
Zidane
Nyota wa zamani wa Ufaransa, Zidane amezungumza
mara kwa mara, kama anayeongozwa, kuhusu usajili wa wa majira ya joto kuhusu
mchezaji anamzimikia dhidi ya washindani wake.Na Pogba pia amekuwa mwangalifu wa kuchagua maneno pindi anapoulizwa kama atapendelea kurudi katika klabu yake ya zamani, United au atajiunga na Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Ohio kabla ya mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Paris Saint-Germain, Zidane aliulizwa kama kuna nafasi yoyote sasa kwa Pogba kutua Bernabeu kabla ya siku ya mwisho ya usajili wa msimu wa majira ya joto hapo Agosti 31.
"Sijui. Kwa sasa tuko hapa tunafanya kazi," alijibu. " Hadi (Agosti 31) chochote kinaweza kutokea. Bado hajawa mchezaji wa Madrid. Hatutaki kuzungumza nini kitatokea."
Wakala wa Pogba, Raiola
Madrid inaonekana haitaki kulipa
Euro 120 milioni kama ingekuwa tayari ingeanza kukusanya pesa kwa kuwauza
baadhi ya wachezaji wake kamaJames Rodriguez au Alvaro Morata.Alipoulizwa kama alishamwomba Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kumsajili Pogba, Zidane alisema: "sasa siyo muda wa kuzungumza kuhusu hilo.
"Kila mmoja anavutiwa na Pogba. Ni mchezaji mkubwa na ukiwa Madrid, siku zote utataka kuwa na kitu kilichokuwa bora. Kwa sasa tunatakiwa kuheshimu baadhi ya mambo- kwa kuwa ni mchezaji wa Juve. Leo sitasema chochote."
Kocha Zidane aliongeza ilikuwa ni vigumu lakini siyo kama haiwezekani kwa nafasi iliyonayo klabu kama Real Madrid, iliyoshinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka mitatu, kumsajili mchezaji na kuendelea kumwendeleza.
"Ni vigumu kukikuza kikosi cha Madrid. Tumeshinda Ligi ya Mabingwa na kikosi hiki," alisema.
Post a Comment