0


SHENZHEN,CHINA
PEP GUARDIOLA amewapiga marufuku wachezaji wenye uzito mkubwa ndani ya Manchester United kufanya mazoezi katika kikosi cha kwanza.
Na kama vile haitoshi amepiga marufuku vyakula vinavyosababisha unene wakati akianza kibarua chake cha kuwanoa wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu.
Bosi huyo wa City hakupoteza muda wa kuweka sheria kali kama zile zilizomsaidia kufanya vizuri akiwa na Barcelona na Bayern Munich kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti kwa ajili ya msimu mpya.

Kiungo mshambuliaji, Samir Nasri ,29, ni mmoja kati ya wachezaji ambao Guardiola alioagiza wapungue uzito kabla ya kujiunga na wenzake wa kikosi cha kwanza. 

Kocha Guardiola yuko makini katika kufuatilia mlo wa wachezaji ‘dayati’ akiwa ameweka kizuizi kwa juisi za matunda zenye karoli nyingi, pizza na vyakula vyote vya kusindikwa.
Beki Gael Clichy ameweka wazi kwamba mchezaji yeyote atakayeshindwa kufikia matakwa ya Guardiola hatakuwamo kwenye kikosi cha kwanza hadi atakapokuwa na uzito unaokubalika.  

“Bila shaka mmesikia kocha alichokisema kuwa na afya nzuri ni kitu muhimu,” alisema Clichy. “Kwake, kama uzito wako ni uko juu zaidi, hutaruhusiwa kufanya mazoezi na timu. Hicho ni kitu cha kwanza.
“Mnaweza kusikia mengi lakini kwa upande wangu, ni mara ya  kwanza kushuhudia kwa kocha yeyote akifanya hivi. Kwa hiyo tunao baadhi ya wachezaji tayari hawafanyi mazoezi na timu.
“Unatakiwa kujua kwamba kama uzito wako ni kilo 60 na una kilo 70, huwezi kucheza soka kwa sababu unaweza kupata majeraha na ukaiingiza timu kwenye matatizo. Hilo ni muhimu.
“Amekataza baadhi ya juisi na bila shaka pizza na vyakula vyote vizito haviruhusiwi. Baadhi ya watu wanadhani vitu hivyo ni vya kawaida lakini kwa kweli, huwa haiwi kama hivi.

“Nafahamu kwa sababu nimekuwa mchezaji soka kwa muda mrefu. Ni kweli inafurahisha na kusisimua sana.
Beki huyo wa pembeni wa wa zamani wa Arsenal na Ufaransa mwenye umri wa miaka, 31, Jumanne amevutwa na ufundishaji wa Guardiola, ambao umemkumbusha bosi wake wa zamani Arsene Wenger.

“Nadhani yeye ni kocha bora kwa kila aina ya mchezaji,' alisema Clichy, ambaye alikuwa Shenzhen sambamba na timu kwa ajili ya mchezo wa Alhamisi dhidi ya Borussia Dortmund.
“Kipa anatakiwa kuwa bora pamoja na uwezo wa kutumia miguu, mabeki wa kati wamekuwa na kiwango kizurina  mabeki wa pembeni wamekuwa na umuhimu.

“Alisema kama angeweza kuwachezesha viungo 11, angewachezesha. Safu ya kiungo iko vizuri. Na washambuliaji watafunga mabao mengi kwa sababu tutatengeneza nafasi za kutosha.

Post a Comment

 
Top