0


RIO DE JANEIRO, BRAZIL
NEYMA amewashukia watu wanaoiponda staili yake ya maisha, akiwauliza waandishi: "Kwa nini nisienda kufurahisa maisha?"
Fowadi huyo wa Barcelona, 24, amekosa michuano ya Copa America yaliyofanyika katika msimu wa majira ya joto, mjini Centenario, Marekani kwa ajili ya kujiandaa kucheza michezo ya Olimpiki itakayoanza mwezi ujao mjini Rio de Janeiro.
Pamoja na kuwa nje ya mashindano hayo ya Copa America, alikuwapo Marekani na alishtumiwa kwa tabia yake ya kutokuwepo uwanjani.

Neymar aliandaa pati katika bwawa la kuogelea na kuangalia mchezo ulioisha kwa sare dhidi ya Ecuador akiwa na sambamba na Justin Bieber na  Jamie Foxx.
Na kama haitoshi alizua mjadala baada ya kuposti kwenye Mtandao wa Instragram akiwaambia wakosoaji  wa timu "nendeni kuzimu " baada ya Brazil kutolewa katika hatua za awali.

... akiwa na Bibber
Neymar alikubaliana kwamba lilikuwa ni jukumu lake pale timu ya taifa ya Brazil ilipotolewa  katika Copa Amerika mwaka 2015,  kutokana na suala lake la kinidhamu lililosabisha kuondolewa mapema, lakini alisema tabia zake za majira haya ya joto siyo jambo la kufanywa kuwa mjadala wa wazi katika jamii.
"Mnatakiwa kuangalia mambo ninayofanya uwanjani. Kitu kingine chochote ni binafsi," Neymar aliwaambia waandishi wa habari.
"Pindi ninapokuwa nje ya uwanja, hayo ni maisha yangu binafsi. Mnatakiwa mnihukumu uwanjani. Sina tatizo kuzungumziwa kuhusu  kadi au kutolewa nje, lakini nina maisha binafsi.  Nina umri wa miaka 24.

.... akiwa na Selana Williams
"Nina mafaniko yangu na nina mambo yangu nje ya hayo. Niko kimya sana kuhusu mambo hayo, lakini bila shaka mnaweza kunikosoa. Nafanya makosa pia. Miye sijakamilika.
"Pia, ninapenda kwenda kufurahi na marafiki zangu. Nina familia na marafiki. Kwa nini nisiende kwenye pati? Ninaweza kwenda na niataendelea kufanya hivyo. Kama nitakuwa makini kwa jukumu langu siku inayofuata, sioni tatizo."
Neymar aliongeza: " Fikiria una miaka 24, unapata kile ninachokipata na unakuwa na kila kitu nilichokuwa nacho. Hutakuwa sawa na mimi?"

Timu ya taifa ya Brazil, itakutana na Afrika Kusini, Iraq na Denmark  katika Kundi A, haijawahi kushinda medali ya dhahabu katika Olimpiki katika mashindano ya soka.
Neymar aliyekuwa mmoja kati ya wachezaji walioambulia medali ya fedha katika mashindano ya mwaka 2012  jijini London alisema: "Sihofii kushindwa.
"Kuwa na hofu ya kushindwa inakufanya uwe na tamaa ya kushinda. Kama tutapoteza, tutapoteza na vichwa vyetu vikiwa juu na tutaendelea, lakini kama itakuwa hivyo, itakuwa ni jukumu langu kufanya kinachowezekana kushinda.
"Sitaki kupoteza. Kupoteza hakupo kwenye fikra zangu. Nataka kuipa Brazil medali ya dhahabu kwani imekuwa vigumu sana."

Post a Comment

 
Top