0


LOS ANGELES, MAREKANI
ARSENE WENGER ameuita usajili wa Paul Pogba anayetarajiwa kutua Manchester United kwa Pauni 100 milioni kuwa ni uwendawazimu.
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Pogba yuko katika hatua za mwisho za kuvunja rekodi akitoka Juventus na kutua na United katika dili ambalo lina thamani zaidi ya Pauni 100 ikiwemo na ada ya wakala.
Pindi alipoulizwa kuhusu gharama za kiungo huyo wa Ufaransa, Wenger alisema: "Moja kwa moja ni uwendawazimu kama huwezi kulipa kiasi hicho. Kama unaweza kumudu kulipa unaweza kuhalalisha.
"Ni uwendawazimu kabisa ulikilinganisha na maisha ya kawaida. Hilo ni kwa uhakika. Lakini tunaishi katika dunia  ambako kila shughuli ulimwengu inatengeneza  kiasi kikubwa cha fedha.
"Soka limekuwa na ushindani ulimwenguni na ndio maana klabu zinaweza kumudu kufanya hivyo, haingii akilini kwamba mchezaji anaweza kurudisha uwekazaji kama huo? Hakuna anayeweza kupiga hesabu.

"Tangu nilipokuwa katika michezo nilikuwa nafikiria kwamba rekodi haziwezi kupanda kumbe sikuwa sahihi. Labda katika miaka michache itafikia 200, 300 (million), nani anajua."
Wenger alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Jumapili kabla ya mchezo wa maandalizi ya msimu dhidi ya Klabu ya Mexico, Chivas jijini Los Angeles.
Mfaransa huyo ambaye mpaka sasa amefanya usajili mkubwa katika dirisha hili la majira joto kwa kumsajili, Granit Xhaka, amedai bado anataka kusajili fowadi na beki wa  kati, lakini ni vigumu kuwapata wachezaji wazuri sokoni.

Post a Comment

 
Top