0


CALFONIA, MAREKANI
JAMIE VARDY hatimaye amevunja ukimya kuhusu uamuzi wake wa kuchagua kubaki Leicester City badala ya kujiunga na Arsenal– akidai hajawahi kuzungumza na Arsenal kuhusu uhamisho.
Straika huyo wa zamani wa Fleetwood, 29, alidai alihisi alikuwa na mengi ambayo hakuwa ameyamaliza katika kikosi cha Foxes.

Vardy ambaye alikosa mchezo wa kichapo dhidi ya Paris Saint-Germain –alisema: “Kila siku nimekuwa nikisema udugu uliokuwapo ndani ya Leicester sio wa kawada.
“Binafsi ninafikiria nina mengi ambayo sijayamaliza hapa. Haukuwa uamuzi mgumu, ulikuwa rahisi, sehemu hii ndio niliyotaka kuendelea kuwepo.”
Alipoulizwa kuhusu sakata lake la muda mrefu kati yake na Arsenal, Vardy alidai kwamba  kwa muda huo akili yake ililenga kwenye michuano ya Euro 2016 na hakuwahi kufanya mazungumzo na Arsene Wenger.
Alisema: “Nilikuwa nje na England. Hapana (sikuzungumza nao).”

Akizungumza zaidi, Vardy anadhani mchezaji mwenzake Riyad Mahrez­, atabakia uwanjani King Power- lakini anajua uamuzi uko nje yamkono yake.
Straika huyo wa England, 29, aliongeza: “Nadhani kila mmoja katika kikosi anamhitaji (Mahrez) aendelee kucheza nasi.
“Lakini hatuna la kufanya ni suala ambalo lipo kwa Riyad na kwa klabu.”

Post a Comment

 
Top