MANCHESTER,
ENGLAND
KINACHOCHELEWESHA
dili la Paul Pogba kukamilika klabuni Manchester United imetajwa kuwa ni cha
juu anachotaka kulipwa wakala wake, Mino Raiola.
Imeelezwa
kwamba Man United imeamua kuvutavuta kidogo kuhusu kukamilisha dili la uhamisho
wa mchezaji huyo, ambaye ataweka rekodi mpya duniani kama uhamisho huo
utafanyika. Man United na Juventus zimeripotiwa kukubaliana ada ya Pauni 105
milioni, kiasi ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya uhamisho wa
wachezaji duniani.
Imeelezwa
kwamba wakala Raiola, ambaye ameamua kupanda ndege kwenda Miami, Marekani
kujadili ishu za mwisho na Pogba kabla ya kuthibitisha uhamisho huo anataka
alipwe cha juu kiasi cha Pauni 18.4 milioni, pesa ambayo Juve walisema wao
hawapo tayari kumlipa wakala huyo labda kama tu Man United watamlipa wao.
Mino Raiola
Juventus ambayo juzi Jumamosi ilifikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain kwa ada ya Pauni 78 milioni, ilisema haipo tayari kulipa cha juu anachotaka kulipwa Raiola, kiasi cha asilimia 20 hivyo kama Man United wanataka dili hilo likamilike, itabidi wao wamlipe wakala huyo.
Kocha Jose Mourinho
Raiola
alikula cha juu wakati alipomhamisha Poga kwenda Juventus mwaka 2012, alibamba
tena pesa ya cha juu wakati kiungo huyo wa Kifaransa aliposaini mkataba mpya na
miamba hiyo ya Turin na sasa anawataka Juve wampe asilimia 20 ya mkwanja ambao
watavuta kwenye uhamisho wa mchezaji huyo kama cha juu chake, jambo ambalo
Juventus wamefichua kwamba hawaoni kama Pogba ana thamani hiyo labda kama tu
Man United watamlipa wakala huyo.
Post a Comment