LIVERPOOL,
ENGLAND
IMEVUJA
aisee. Ndiyo hivyo, siri za kambi ya timu ya Liverpool kwenye hoteli yao
imevuja na kuelezwa mambo mbalimbali wanayotaka mastaa wa kikosi hicho cha
Anfield kinachonolewa na Jurgen Klopp.
Wakati
Liverpool ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England sambamba na kucheza
mechi kibao za kirafiki, kwenye hoteli waliyofikia nyota wake wametoa masharti
ambayo sasa yamevuja na kufahamika kwenye mitandao ya kijamii.
Miongoni
mwa matakwa ya kushangaza waliyotaka wachezaji wa Liverpool kwenye hoteli
waliyoweka kambi, kwamba nahodha wa kikosi, Jordan Henderson ametaka chumba
chake kiwe karibu na Adam Lallana, wakati kocha Klopp ni lazima apewe chumba
chenye hadhi kubwa ambacho kinaruhusu kuvuta sigara na moshi usiendelee kubaki
chumbani kwa muda mrefu.
Philippe
Coutinho chumba chake kisiwe na kipoza hewa bali kiwa na feni na kwamba vilevi
vyote pamoja na vitu vya kutafunatafuna viondolewe kwenye vyumba vya wachezaji.
Matakwa ya wachezaji hao yote yamewekwa kwenye video moja ambayo imekuwa
ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kikosi cha Liverpool kwa sasa kipo
Marekani ambako kitacheza mechi na Chelsea, AC Milan na AS Roma.
Post a Comment