LONDON,
ENGLAND
MASHABIKI
wa Arsenal wamemtaka kocha wao, Arsene Wenger kumsajili mshambuliaji wa
Manchester United, Anthony Martial.
Fowadi
huyo Mfaransa, Martial ameripotiwa kuchukizwa na kitendo cha kuporwa Namba 9
klabuni Man United na kupewa Zlatan Ibrahimovic bila ya kuelezwa chochote.
Mashabiki
wa Arsenal sasa wanamtaka kocha wao kuchangamkia fursa hiyo ili kumnasa
Martial, ambaye msimu uliopita alionyesha kiwango kizuri klabuni hapo. Man
United ilimnasa mchezaji huyo kutoka Monaco kwa ada ya Pauni 36 milioni.
Alifunga
bao maridadi kabisa katika mechi yake ya kwanza Man United ilipocheza dhidi ya
mahasimu wao Liverpool na tangu hapo akajitengenea nafasi katika kikosi cha
kwanza cha miamba hiyo ya Old Trafford.
Lakini,
ujio wa kocha mpya klabuni hapo, Jose Mourinho na straika Ibrahimovic
limemfanya Martial kunyang’wanya jezi Namba 9 na kupewa jezi yenye Namba 11,
hivyo mashabiki wa Arsenal walitumia kurasa zao za mtandao wa Twitter kumweleza
kocha huyo amsajili straika huyo atawasaidia sana msimu ujao.
Mashabiki
hao wanamtaka Wenger amnase fowadi huyo na kumkabidhi jezi Namba 9 ambayo
aliporwa huko Old Trafford.
Post a Comment