0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO ametua uwanjani Carrington kwa mara ya kwanza kwa ajiri ya kuanza kazi ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kocha huyo amerithi kikosi chenye vipaji ambacho kitaongezewa wakali wapya wakiwamo, straika Zlatan Ibrahimovic, kiungo, Henrikh Mkhitaryan na beki Eric Bailly ambao watatakiwa kusaidia kufanya kazi ngumu ya kusaka ubingwa.
Mourinho aliingia uwanjani hapo akiambatana na kocha msaidizi, Rui Faria na wa makipa, Silvino Louro, ingawaje hakukuwa na dalili ya kuwapo kwa kipa David de Gea, ambaye bado yuko kwenye mapumziko kufuatia kushiriki Euro 2016.


Kocha Mourinho na msaidizi wake Rui Faria
Wachezaji Wayne Rooney, Chris Smalling, Anthony Martial, Maroune Fellaini, Marcus Rashford, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin na  Bastian Schweinsteiger pia walikuwa kwenye mapumziko hayo.

Wachezaji wa United waliofika mazoezini kwa ajili ya kuthibitisha uwezo wao kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England waliongozwa na, Juan Mata, ambaye Mourinho alimuuza walipokuwa Chelsea.

Mata itambidi kupambana katika ipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao, kwa ajili ya kubaki United, kama ilivyo kwa Daley Blind, Ander Herrera na Memphis Depay kufuatia kununuliwa kwa gharama kubwa. 
Kocha Mourinho anatarajiwa kukipunguza kikosi chake na kuwa na wachezaji 24, na yeyote atakayeachwa atatakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha U-21 au kutolewa kwa mkopo.

Mbali na Blind na Mata, beki wa Kiargentina, Marcos Rojo anatakiwa kupigania nafasi mbele ya Guilermo Varela, beki Tyler Blackett amesharudishwa kwenye kikosi cha vijana, wakati James Wilson bado yupo kwenye kikosi cha kwanza  wakati huu Kocha Mourinho akiwasubiri nyota wake wa kimataifa. 


Mchezaji mpya, Mkhitaryan akifanya mazoezi na Adnan Januzaj

Kitu cha kuvutia kwenye mazoezi hayo kilikuwa ni kurejea kwa beki, Luke Shaw, ambaye anajipanga kucheza mchezo wa maandalizi wa msimu wa kirafiki dhidi ya Wigan, Jumamosi baada ya miezi 10 iliyopita kuuguza mguu wake alioumia mwezi Oktoba. 
Wakati United ikimpoteza mzoefu wake mwenye miaka 29 katika klabu, kufuatia kuondoka kwa Ryan Giggs, bado kutakuwepo mkongwe mwingine mwenye umri wa miaka 35, Michael Carrick baada ya kukubali kusaini dili la mwaka mmoja.

Kocha Mourinho ataendelea kusubiri nafasi ya kufanya kazi na  nahodha wa England, Rooney, ambaye yuko mapumzikoni na straika huyo ana  hamu ya kuona Mreno huyo amepanga mikakati gani kwa ajili yake.
“Nina furaha kufanya kazi na Jose msimu huu kama mmoja kati ya makocha bora duniani,” Rooney alikaririwa.
Kocha Mourinho alikaririwa akipinga kitendo cha Rooney kuchezeshwa  katika nafasi ya kiungo akiwa na timu ya taifa.
Kutakuwa na mabadiliko katika viwanja vya mazoezi vya Carrington katika wiki na miezi ijayo, wakati Mourinho akiweka alama zake klabuni hapo. 


Usajili mpya, Eric Bailly (kulia) akiwa na straika Will Keane uwanjani Carrington

Tayari Mreno huyo ametaka kuondolewa kwa kamera zilizokuwa zikiwaangazia wachezaji wavivu mazoezini zilizowekwa na mtangulizi wake, Luios van Gaal, akisema ana uwezo wa kuwaona wachezaji wavivu bila ya kutumia kamera.

Post a Comment

 
Top