STAMBULY, UTURUKI
MARTIN SKRTEL amefuzu vipimo vya
afya akiwa katika harakati za kutua klabuni Fenerbahce.Awali ilikaripotiwa kwamba, ada inayokadiriwa kuwa Pauni 5 milioni ilikubaliwa na Skrtel alipewa ruhusa ya kufanya mazungumzo na Fenerbahce.
Beki huyo wa kati aliwasili Uturuki Jumanne kumalizia uhamisho wake kwa washindi wa pili hao wa msimu uliopita.
Skrtel ambaye alisaini mkataba mpya na Liverpool Julai 2015, amejikuta nje kikosi cha kwanza cha Kocha Jurgen Klopp.
Kuwasili kwa Joel Matip kutoka Schalke na kukaribia kurudi kwa kinda Joe Gomez kuliongeza ushindani katika kikosi hicho cha Anfield.
Beki huyo wa Slovakia alijiunga na Liverpool Januari 2008 na amecheza mechi 320 akiwa na Wekundu hao.
Post a Comment