LONDON,
ENGLAND
ANTONIO
CONTE Jumatano aliwasili rasmi kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea kwa ajili ya
kuanza kazi ya kuinoa miamba hiyo ya Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu England.
Mtaliano
huyo mwenye umri wa miaka 46, alionekana akiwa ndani ya ndinga yake akielekea
kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea, Cobham tayari kwa ajili ya kuanza mambo ya
kutengeneza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Conte,
ambaye aliifikisha Italia katika hatua ya robo fainali ya Euro 206, na kupoteza
mchezo huo kwa mikwaju ya penalti na Ujerumani, ana changamoto ya kuirejesha
Chelsea katika makali yake baada ya kuboronga msimu uliopita.
Katika
siku yake ya kwanza mazoezini, kumeibuka ripoti kwamba Chelsea inakaribia
kwenye dili la kumsajili kiungo wa Leicester City, N'Golo Kante. Miamba hiyo ya
Stamford Bridge tayari imeshamwongeza fowadi moja kwenye kikosi chake, Michy
Batshuayi, iliyomnasa kwa ada ya Pauni 33 milioni, huku ikimwongezea pia
mkataba mpya Mbrazili, Willian.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Conte kuinoa timu ya England sawa na ilivyo kwa Pep
Guardiola, atakayekuwa na kikosi cha Manchester City msimu ujao.
Post a Comment