0


LONDON, ENGLAND
SAM ALLARDYCE amekubali miaka miwili ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England –baada ya klabu yake ya Sunderland kukubali  fidia ya FA ya Pauni 3 million na kumruhusu kuonodoka.
Maofisa FA walitumia siku mbili kukubaliana kiasi na ‘Black Cats’ baada ya kuamua Allardyce ni mtu sahihi wa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Roy Hodgson.
Na walifikia makubaliano ya mwisho asubuhi ya Ijumaa– na kumthibitisha kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 mchana .
Atakuwa na kibarua cha kuiongoza England kwenda Kombe la Dunia Urusi mwaka  2018 na kufanya mambo mazuri zaidi ya mtangulizi wake alivyofanya kwenye Euro 2016 na Kombe la Dunia 2014.

Kocha Allardyce, atamchagua Sammy Lee kuwa msaidizi wake alisema : “Nimepewa heshima kubwa kuchaguliwa kuwa kocha  wa England hasa kwa kuwa hakuna siri, hilo ndilo jambo ambalo siku zote nimekuwa nikilitaka.
“Kwangu, bila shaka ni kazi bora katika soka la England.
"Nitafanya kila kitu kuisaidia England kufanya vizuri na kulipa taifa letu heshimba ambayo mashabiki wanastahili.
"Juu ya yote, tutawafanya watu na nchi nzima kujisikia fahari."
Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn alisema: "Sam Allardyce ni mtu sahihi kwa kibarua cha kuinoa England.

"Usimamizi katika uongozi wake, vikiwemo na kipaji chake cha kutambua uwezo wa wachezaji na timu, kujenga timu yenye nguvu na kukumbatia mbinu katika soka la kisasa ili kuongeza utendaji, vimemfanya awe chaguo bora.”

Post a Comment

 
Top