LONDON, ENGLAND
ANTONIO CONTE ameweka wazi kwamba
straika wake Diego Costa kamwe hauzwi.Costa mzaliwa wa Brazil mara kwa mara amekuwa akihusishwa na mpango wa kurejea Atletico Madrid ambako aliitumikia klabu hiyo kwa miaka sita kabla kabla ya kutua London ya Magharibi na kutamba kwa misimu miwili.
Kwa siri Atletico imekuwa ikifanya jitihada za kumrudisha straika huyo Calderón, huku nahodha wa klabu hiyo, Gabi akiwa mmoja kati ya wachezaji wa zamani wanaowasiliana na Costa kwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumshawishi kurudi.
Costa alipokuwa na Atletico Madrid
Tetesi zilizozagaa Jumatatu jioni ni
kwamba Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo aliweka wazi kwamba wanalifanyia
kazi dili la mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kurudi Vicente Calderon.Lakini Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anamuona Costa ni sehemu kati ya wachezaji waliopo katika mipango yake, na amesisitiza hayuko katika shinikizo la kumuuza.
Costa akiwa na Chelsea
Akizungumza kwenye mkutano wa
waandishi wa habari Jumanne iliyopita, kocha
huyo wa zamani wa Juventus ya Italia alisema: "Diego Costa ni mchezaji
wetu, ni mchezaji mzuri aliye na umuhimu mkubwa sana. Ana furaha na ni
mchapakazi kwelikweli."
...Kocha Conte
Aidha Conte alisema winga wa
Colombia, Juan Cuadrado atapewa nafasi ya kuonesha uwezo wake kabla ya
kuchukuliwa uamuzi mwingine mbele ya safari.Alisema: "Cuadrado ni mchezaji wa Chelsea. Nampenda. Amewasili leo na mchana ameanza mazoezi."
Post a Comment