0


SHANGHAI, CHINA
MANCHESTER UNITED imepata kichapo cha kwanza cha mabao 4-1 dhidi ya Borussia Dortmund Shanghai, China huku Henrikh Mkhitaryan akifunga dhidi ya timu yake ya zamani.
Kabla ya mchezo huo, kocha wa United, Jose Mourinho alisema matokeo siyo muhimu lakini kipigo hicho cha kwanza kinaweza kumtia wasiwasi.

Wakati Mkhitaryan akifunga bao lake, United ilikuwa nyuma kwa mabao 3-0, huku Dortmund ikionyesha kwa jinsi gani ilikuwa vizuri, na mashambulizi yake makali na ikiuvunjavunja ukuta wa Man United uliokuwa ukicheza kwa kujihami.
Gonzalo Castro alifunga mara  mbili, ikiwemo moja la juhudi binafsi za Pierre-Emerick Aubameyang ambaye naye alifunga moja na Ousmane Dembele alifunga lingine.

Ulikuwa ni wakati mwingine mbaya wa Memphis Depay,ambaye alishindwa kufanya vizuri, pamoja na kupewa nafasi ya kucheza mbele. Phil Jones pia alianza katika kikosi cha United akiwa beki wa kati lakini hakuonesha kiwango cha kushawishi.

Ilikuwa siku nzuri kwa Juan Mata, ambaye alimaliza mchezo huo akiwa nahodha – kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Wigan Jumamosi- ambapo alitengeneza bao la kwanza.
Mourinho hakuwa amepanga kumtumia Marcus Rashford katika viwanja vya China, lakini alimwingiza baada ya mapumziko wakati United ikitaka kusawazisha mabao.  Hatimaye United ilipata bao baada ya Mata kutoa asisti kwa Mkhitaryan.

Post a Comment

 
Top