PARIS,
UFARANSA
CRISTIANO
RONALDO nyota yake imeweka huku ile ya hasimu wake, Lionel Messi akianguka- baada
ya kushinda mataji yenye hadhi ya kimataifa.
Wachezaji hao wakubwa wa kizazi hiki
wana heshima katika nchi zao, mbali na kuzua mijadala duniani.Straika Lionel Messi amebeba tuzo ya Ballon D’or mara tano na Ronaldo mara tatu. Baadhi ya wadau wa soka wanaamini kwa heshima hii, Mreno huyo ataongeza tuzo ya nne.
Ronaldo ameshinda taji. Ureno iliifunga Ufaransa kupitia bao la Eder katika dakika108 . Ureno imefika nusu fainali ya Kombe la Dunia mara mbili na ilifika fainali ya Euro mwaka 2004.
Lakini sasa imefika fainali na kufanikiwa.
Katika mashindano yake ya 13 ya kimataifa na imepiga hatua.
Argentina ya Messi, ina utajiri wa historia katika soka.
Mara mbili imetwaa Kombe la Dunia mwaka 1978 na mwaka 1986 na imekuwa bingwa wa Copa Amerika mara 14.
Hata hivyo, haijashinda chochote tangu mwaka 1993. Na ikiwa na Messi, Argentina imemaliza katika nafasi ya pili katika miaka minne ndani ya maika mitano katika mashindano ya Marekani ya Kusini – kama ilivyokuwa mwaka 2014 katika Kombe la Dunia.
Baada ya mshtuko wa penalti mwaka huu katika Copa Amerika, straika huyo wa Barcelona, alitangaza kustaafu mashindano ya kimataifa- akiwa hana heshima.
Ronaldo mpaka sasa amecheza katika mashindano saba makubwa na hatimaye ameshinda moja.
Nyota huyo anaweza kuongeza na medali ya dhahabu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyoshinda na Real Madrid mapema msimu huu.
Pamoja na kwamba alitoka baada ya dakika ya 25 katika fainali ya Jumapili, Ronaldo amefanya kweli. Amevaa dhahabu akiwa na Ureno.
Post a Comment