MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO (pichani juu) atawapiga
panga wachezaji wanane wa kikosi cha sasa wakati akipambana kumsajili nyota wa Juventus,
Paul Pogba.
Bosi huyo wa Manchester United anataka
kufanya kazi na kikosi cha wanaume 22 ili kujenga msingi wa timu.Kiungo Pogba, 23, atanaswa kwa Pauni 100 milioni akiwa ni sehemu ya kocha huyo maarufu kama Special One kufanya mageuzi Old Trafford. Ili kutimiza mkakati huo baada ya wachezaji watauzwa na wengine watatolewa kwa mkopo.
Chanzo ndani ya United kimesema: “Jose ameweka wazi kwamba anataka kufanya kazi na wachezaji muhimu 22. Hiyo inamaanisha wanane itabidi waondoke.”
Wachezaji Marcos Rojo, Morgan Schneiderlin na Bastian Schweinsteiger wako katika hatari kwa kuwa wamekuwa na msimu mbaya.
Wengine Adnan Januzaj alitolewa kwa mkopo msimu uliopita na wasiwasi zaidi uko kwa Memphis Depay, Daley Blind na Juan Mata (pichani juu).
Kocha Mourinho anakwenda sambamba na klabu yake ya zamani ya Real Madrid ambayo nayo inajaribu kumsajili Pogba (pichani chini).
United tayari imeshafanya biashara na wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa Mino Raiola katika msimu huu wa majira ya joto na kuwachukua Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.
Post a Comment