MANCHESTER, ENGLAND
PAUL POGBA amerudi
klabuni Manchester United kwa mara nyingine baada ya kukubaliwa dili la
uhamisho la Pauni 100 milioni usiku wa Alhamisi.
Kiungo huyo wa
Ufaransa amekubali kusaini mkataba wa
miaka mitano na atakuwa akulipwa mshahara wa Pauni 290,000 milioni kwa wiki.
Dili hilo
limekamilika baada ya wiki kadhaa za majadiliano na United kukubali kulipa
kiasi hicho kikubwa kwa ajili ya nyota huyo wa Juventus ili kukamilisha usajili
wa majira ya joto wa kocha wao, Jose Mourinho.
United ilikuwa na
hamu ya kumsainisha nyota huyo- aliyekamilisha zoezi la vipimo vya afya jijini Los
Angeles na atapewa jezi namba 6 – huku akisubiri utambulisho rasmi.
Dili la kiungo huyo mwenye
umri wa miaka 23 limefanyika baada ya wakala wa
Pogba, Mino Raiola kufanya mazungumzo na maofisa na wanasheria wa Juventus
jijini Turin Alhamisi mchana.
United na Juventus zimekubaliana
kumlipa bonasi ya asiliamia 20 Raiola katika sehemu ya jumla ya dili hilo la Pogba.
Inafahamika kwamba, Juventus
itatangaza ada ya Pauni 84.3milioni kutoakana na kodi wanayotakiwa kulipa. Rekodi
kubwa ya uhamisho duniani ni Pauni 86 milioni iliyolipwa na Real Madrid kwa
Tottenham kwa ajili ya kumnasa Gareth Bale mwaka 2013.
Pogba alifanyiwa
vipimo vya afya Los Angeles baada ya kumaliza
mapumziko Florida kabla ya kusaini dili hilo.
Malipo mengine
yaliyokubaliwa kati ya klabu hizo ni bonasi kwa Juventus pindi Pogba atakaposaini
mkataba mpya United na akishinda tuzo ya Ballon d'Or.
Nyota huyo wa
Ufaransa alinaswa katika duka kubwa la Beverly HIlls Alhamisi alipoenda kununua
jozi ya viatu na alifika katika Mgahawa maarufu wa Kichina wa Mr Chow.
Pogba aliondoka Old
Trafford Julai, 2012 baada ya Kocha wa United, Sir Alex Ferguson alipokataa
maombi ya Raiola ya kumuongezea mkataba. Juventus ililipa fidia ya Pauni 800,000.
Huu utakuwa ni usajili
wa nne kwa United tangu Mourinho
alipochaguliwa kuwa kocha mpya, ukifuatiwa na beki Eric Bailly, straika Zlatan
Ibrahimovic na kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan.
Rekodi kubwa kulipwa
na klabu ya Kiingereza ilikuwa ni Pauni 59.7 milioni pale United ilipomchukua Winga
wa Kiargentina, Angel Di Maria kutoka Real Madrid Agosti 2014.
Habari zilipatikana
baada ya dili hilo kukamilika zinadai kwamba Mourinho atamtosa Mjerumani,
Bastian Schweinsteiger ,31, au atamtoa kwa mkopo.
Post a Comment