0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO hataki mchezo kabisa, amefanya kikao na wachezaji wote na tisa kati yao kuwataka waondoke mara baada ya dili la Paul Pogba kukamilika.
Baada ya kiungo huyo wa Juventus kukubali dili la miaka mitano Old Traffold, Mourinho aliwaonya nyota hao kwamba hawatakuwa na maisha marefu klabuni hapo.

Majeruhi wa kwanza wa katika uchinjwaji huo wa kikatili wa Manchester United atakuwa kiungo Bastian Schweinsteiger.
Mjerumani Schweinsteiger, 31, anawezaa kukatwa na Mourinho kwa ajili ya kuuzwa au kutolewa kwa mkopo, sambamba na makinda wengine wanane.

Cameron
Beki wa kushoto, Tyler Blackett, 22, na straika James Wilson, 20, wataruhusiwa kuondoka, sambamba na mshambuliaji, Will Keane, 23 ambaye bosi mpya wa Sunderland, David Moyes ameonesha kuvutiwa naye.

Pereira
Kinda wa Kibrazili kiungo, Andreas Pereira, 20, pia anaweza kulimwa na kutokuwa na maisha marefu United.
Hata makinda yaliyokuzwa Old Trafford mabeki pacha, Paddy McNair, 21, na Cameron Borthwick-Jackson, 19, wako katika wakati mgumu wakati Mbelgiji, Adnan Januzaj, 21, amejawa na hofu ya kukatwa pia.

Kean
Tayari beki wa kulia wa raia wa Uruguay, Guillermo Varela, 23, ameshajiunga na klabu ya  Eintracht Frankfurt baada ya kutolewa kwa mkopo.
Beki wa Mholanzi, Timothy Fosu-Mensah, 18, atabaki kwa kuwa ameshapewa mkataba mpya.

Januzaj
Julai 10, mwaka huu Mourinho aliweka wazi kwamba anahitaji kufanya kazi na wachezaji 22 kwa ajili ya msimu ujao.
Na Alhamisi kocha huyo alifanya mkutano na wachezaji wote ambao hawako katika mipango yake msimu ujao.

Post a Comment

 
Top