0



MANCHESTER, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC straika mpya wa Manchester United atakosa michezo ya maandalizi ya msimu katika ziara ya China itakayofanywa na klabu hiyo wiki hii, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.
Taarifa hizo zinasema kwamba, Jose Mourinho anaweza kumpa ruhusa Ibrahimovic, 34, kutosafiri na timu pamoja na kwamba amepata takribani wiki tatu za mapumziko baada ya Euro 2016, kama inavyotakiwa na Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa).

United itapambana na Borussia Dortmund mjini Shanghai Julai 22 na Manchester City jijini Beijing Julai 25, lakini Mourinho anaripotiwa kuwa na mpango wa kumpa nyota huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain nafasi zaidi ya kupumzika kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Ibrahimovic, ambaye alistaafu kucheza michezo ya kimataifa baada ya Sweden kutolewa katika fainali za Euro 2016 katika hatua ya makundi, bado yuko mapumzikoni lakini hivi karibuni alituma video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha akifanya mazoezi kudumisha kiwango chake. 
Inatarajiwa kwamba Ibrahimovic ataweza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Galatasaray utakaochezwa Swedish jijini Gothenburg Julai 30.
United pia inakabiliwa na mchezo wa National League North dhidi ya Salford City inayomilikiwa na magwiji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu, wakongwe, Gary Neville na Ryan Giggs Julai 26.

Wachezaji wengine wawili waliosajiliwa katika majira ya joto, MuiIvory Coast beki wa kati, Eric Bailly na kiungo wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, walifanya mazoezi kwa mara ya kwanza Jumatano na wanajipanga kwa kusafiri na kikosi hicho kwenye ziara hiyo ya China.
Beki Luke Shaw, ambaye alikosa michezo mingi ya msimu uliopita baada ya kuvunjika mguu mara mbili, pia alijumuika katika mazoezi hayo.
Wachezaji watatu waliokuwa wakiitumikia England, Wayne Rooney, Chris Smalling na Marcus Rashford watasafiri kwenda China baada ya kuwa mapumziko kufuatia kutolewa katika hatua ya 16 bora ya fainali za Euro 2016, Juni 27 lakini Kocha Mourinho alisema hatawatumia katika michezo hiyo.

Post a Comment

 
Top