LONDON, ENGLAND
ANTONIO CONTE kocha mpya wa Chelsea
amesema nahodha John Terry ataendelea kubaki na kitambaa cha uongozi katika
klabu hiyo, bila ya kujali kama atakuwa akicheza au la.Kocha Conte alithibitishwa kuwa kocha wa Chelsea mwezi wa Aprili, wakati Guus Hiddink akiwa kocha wa muda huku kukiwa na wasiwasi wa mustakabali wa baadaye wa beki Terry klabuni hapo.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 baadaye alimwaga wino wa kuitumikia klabu hiyo kwa mwaka mmoja Mei mwaka huu, lakini awali alikaririwa akisema kwamba angeweza kukubali jukumu lolote ndani ya klabu hiyo.
Hatimaye, Conte ametua Stamford Bridge baada ya kuifikisha Italia katika hatua ya robo fainali ya Euro 2016 na katika mkutano wake wa kwanza, amewaaambia waandishi wa habari: "John Terry amepewa mkataba kama mchezaji, sio kwa ajili ya jukumu lingine tofauti.
"Ni mchezaji mwenye heshima kubwa. Napenda kuzumgumza naye kwa sababu najua kuwa anaijua klabu, ana haki na ushawishi katika klabu, na kwangu ni mchezaji muhimu, kama wengine."
Imekuwa ikidaiwa kuwa Terry atakuwa na ushiriki mdogo katika mipango ya Conte, lakini bosi huyo wa zamani wa Juventus alisema: "Pindi mchezaji anapostahili kucheza, kwangu atacheza."
Kocha Conte alisema, bila ya kujali kama Terry atakuwa kwenye kikosi, atabaki kuwa nahodha wa klabu.
"John Terry ni nahodha wa Chelsea pindi anapocheza na hata asipocheza," alisema. "Ni nahodha wa Chelsea kila siku.”
Alipoulizwa kama alishiriki katika uamuzi wa kumuongezea mkataba wa Terry Chelsea, Conte alikubali.
"Narudia kwamba John Terry ni mchezaji muhimu kwa klabu. Uamuzi wote tulifanya pamoja na klabu.
"Nina furahsa sana. Nimezungumza naye kwa nyakati tofauti na kwangu kilikuwa ni kitu mihimu pindi John aliposajiliwa."
Post a Comment