LONDON,
ENGLAND
BARCELONA
imeelezwa kwamba ndiyo timu yenye safu ya ushambuliaji ghali zaidi duniani.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo ya Michezo
kuhusiana na thamani ya wachezaji sokoni, fowadi ya Barcelona iliyopachikwa
jina la MSN kwa maana ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, inatajwa kuwa na
thamani ya juu zaidi duniani.
Fowadi
hiyo kwa jumla ina thamani ya Pauni 400 milioni, pesa ambayo kama utaichenji
kwa shilingi, basi utapata Shilingi 1,134,720,000,000.
Messi
anaongoza kwa kuwa na thamani ya Pauni 177.15 milioni, lakini kiwango hicho
kikiwa kimepungua kwa Pauni 33.57 milioni kutoka kwenye thamani yake ya awali.
Neymar anamfuatia kwa karibu, akiwa na thamani ya Pauni 169.10 milioni baada ya
kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kubaki Nou Camp.
Staa
mwingine wa fowadi hiyo ya Barcelona, Suarez anashika namba saba kwa kuwa na
thamani ya Pauni 88.79 milioni iliyopanda baada ya kufanya vizuri msimu
uliopita ambapo alifunga mabao 60 katika michuano yote aliyoshiriki.
Supastaa
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye ameifikisha Ureno nusu fainali ya Euro
2016 anashika namba tatu kwa kuwa na thamani ya Pauni 115.64 milioni na hivyo
kuzidiwa na Messi na Neymar.
Kwa
upande wa Ligi Kuu England, mchezaji mwenye thamani kubwa ni kinda wa
Manchester United, Anthony Martial, mwenye thamani ya Pauni 93.82 milioni na
hivyo kushika namba tano duniani, wakati namba nne ni Antoine Griezmann mwenye
thamani ya Pauni 100.87 milioni.
Mastaa
wengine waliopo kwenye 10 bora ni Paulo Dybala wa Juventus mwenye thamani ya
Pauni 87.69 milioni na kufuatiwa na Sergio Aguero wa Manchester City mwenye
thamani ya Pauni 81.23 milioni.
Paul
Pogba yupo kwenye nafasi ya tisa akiwa na thamani ya Pauni 75.86 milioni na
Gareth Bale akikamilisha orodha hiyo ya 10 bora kwa kuwa na thamani ya Pauni
67.81 milioni, soko likishuka kiasi kikubwa sana baada ya usajili wake
kuigharimu Real Madrid Pauni 85 milioni miaka mitatu iliyopita.
Staa
wa Arsenal, Alexis Sanchez ana thamani ya Pauni 63.61 milioni, wakati supastaa
wa Chelsea, Eden Hazard thamani yake ni Pauni 65.71 milioni na kushika nafasi
ya 11.
Kwenye
nafasi ya 13 yupo Mwingereza, Dele Alli wa Tottenham Hotspur, ambaye thamani
yake ni Pauni 63.11 milioni, zaidi ya Thomas Muller wa Bayern Munich anayeshika
nafasi ya 14 kwa kuwa na thamani ya Pauni 61.68 milioni.
Raheem
Sterling wa Manchester City thamani yake ni Pauni 61.09 milioni, wakati Robert
Lewandowski wa Bayern Munich ana thamani ya Pauni 56.90 milioni, akifuatiwa na
Alvaro Morata mwenye thamani ya Pauni 53.88 milioni na Toni Kroos wa Real
Madrid akiwa na thamani ya Pauni 52.20 milioni, huku anayekamilisha nafasi ya
19 ni Gonzalo Higuain wa Napoli mwenye thamani ya Pauni 51.11 milioni.
Hii
ndiyo orodha ya wachezaji 19 wenye thamani kubwa zaidi duniani ukitaka
kuwasajili basi lazima ujipange.
Listi kamili ni hii hapa chini
Post a Comment