0


LIVERPOOL, ENGLAND
JURGEN KLOPP akiwa na sura mpya, sura za zamani, uso wake ulionekana kutabasamu muda wote, wakati Liverpool wakirudi  uwanjani kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, Jumamosi.
Bosi huyo wa Wekundu hao wa Anfield  alionekana kufurahi  na wachezaji wakikimbia katika uwanja wao wa Melwood baada ya mapumziko wa majira ya joto.
Wachezaji wapya, Sadio Mane, Loris Karius, Joel Matip na Marko Grujic walishiriki mazoezi hayo wakati Danny Ings alikuwa akitabasamu baada ya kukaa nje ya uwanja karibu msimu wote uliopita kutokana majeraha.

Straika Mane, amesajili kutoka Southampton kwa Pauni 30 milioni, alikuwa uwanjani hapo tayari kwa ajili ya vita vya Ligi Kuu ambapo Liverpol itaanza dhidi ya Arsenal Agosti 13, ugenini.

Mchezaji aliyekuwa  kwa mkopo AC Milan ya Italia, Mario Balotelli naye alikuwapo kwenye mazoezi hayo ya mwanzo wa msimu.
Kocha Klopp alionekana akifanya utani na kiungo wa Kibrazili, Lucas Leiva.Wachezaji wote wa Liverpool waliokuwa wakishiriki Euro 2016 au Copa Amerika hawakutakiwa kuudhuria baada ya kupewa mapumziko.
Kocha Andreas Kornmayer aliongoza mazoezi hayo katika hatua za awali. 


Post a Comment

 
Top