LONDON,
ENGLAND
DIEGO
COSTA (pichani) amezidi kuing'ang'aniza Chelsea impige bei Atletico Madrid, lakini miamba
hiyo ya Stamford Bridge imemnyamazia na kuamua kuwapiga chini Radamel Falcao na
Alexandre Pato.
Chelsea
imewapiga chini mafowadi wake Falcao na Pato ambao walikuwa klabuni hapo kwa
mkopo huku wakiwa na shida ya kumtuliza Costa, ambaye ameonekana kupania kutaka
kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Chelsea
inakabiliwa na changamoto nyingi kwa fowadi wanayemfukuzia Alvaro Morata baada
ya Real Madrid kuwaambia kwamba dili hilo linaweza kukamilika tena wakawaongezea na pesa kiasi cha Pauni 40
milioni ili wao wamchukue Eden Hazard.
Wachezaji
wengine waliopigwa chini ya Chelsea itakayokuwa chini ya Kocha Antonio Conte
msimu ujao ni kipa Marco Amelia. Mastaa wengine wanaowindwa na Conte ni John
Stones, Stefano Sturano, Antonio Candreva na Romelu Lukaku.
Post a Comment