MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO (pichani juu) amesema wakongwe wa Manchester
United wanaowakosa makocha wa timu hiyo katika vyombo vya habari wanaweza kuwa
na athari kutokana na desturi za mashabiki kuwakubali.Wakongwe Roy Keane, Paul Scholes, Gary Neville, Ryan Giggs, Rio Ferdinand ni baadhi ya nyota wa zamani wa United wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari kwa miaka ya hivi karibuni, na wengi wamekuwa wakitoa maoni yao pindi klabu inapopitia wakati mgumu tangu, Sir Alex Ferguson alipostaafu mwaka 2013.
Wakati huu Mourinho amepondwa katika hatua hii, baada ya Scholes kutengeneza vichwa vya habari mwishoni mwa wiki aliposema kiungo, Paulo Pogba hana thamani ya pesa ambazo United inatarajia kumpa.
Scholes amesema Pogba hana thamani kubwa kihivyo.
Kiungo mkabaji, ‘mgumu’ Owen Hargreaves alikaririwa mwezi uliopita akidai kwamba klabu imetekwa na Wareno.
Kocha Mourinho amekiri kwamba wachezaji wa zamani wana nguvu ya kutengeneza wakati mgumu lakini alikuwa na furaha zaidi kuwakaribisha klabuni.
"Katika klabu hii utakutana na wakongwe kuanzia miaka mitano iliyopita, miaka 10 iliyopita, miaka 15 iliyopita na wa miaka 20 iliyopita," alisema.
"Sauti zao zina nguvu. Hiki ni kitu unachotakiwa kukifahamu. Kwamba watu hao wanahusika na historia ya klabu, wao ni tofauti na wachambuzi wa kawaida. Unatakiwa uwaangalie katika mtazamo tofauti. Unatakiwa uwe na heshima kwa watu hawa.
"Wana nguvu sana katika dunia ya mashabiki wanaweza kuwa na ushawishi mzuri au mbaya. Mashabiki wanawapenda, kwa hiyo wanapokuwa chanya wanaweza kuwaunganisha na wanapokuwa hasi wanaweza kutengeneza hali ngumu.
"Wanafanya kazi na wanatakiwa kujaribu kuwa wakarimu na wategemezi. Kwa hiyo, binafsi kama kocha wa Manchester United siwezi kuwauliza, 'Mnahusika katika historia yetu, mnatakiwa kusaidia.
Pogba siku zake za kutua United zinahesabika
“Unatakiwa ukubali kama watakuwa na
furaha wanaweza kusaidia; Kama hawatakuwa na furaha labda wanaweza kusumbua na
kufanya mambo kuwa magumu."Nitawaambia:, 'Mnakaribishwa kwenye uwanja wa mazoezi.' Wakati wowote mnaotaka kutoa maoni, karibuni, ni nyumbani kwenu, mnaweza kurudi kama mnataka."
Wakongwe hao kwa njia moja ama nyingine walisababisha, makocha David Moyes na Luis van Gaal kutupiwa virago.
Wakati huohuo, Gary Neville amekataa maoni ya kuchukua jukumu la kufundisha katika benchi la ufundi la United, alisema: " Hilo halitaweza kutokea."
Post a Comment